Katika mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Old Trafford Rashford ambaye alifunga mabao mawili katika mchezo wake wa kwanza na timu ya wakubwa dhidi ya FC Midtjylland Alhamisi, alifunga bao la kwanza katika dakika ya 28.
Mchezaji wa zamani wa Manchester United, Danny Welbeck alisawazisha bao na kuirejesha Arsenal katika mchezo, lakini Rashford tena akinasa shuti lililopigwa na Herrera alipachika wavuni bao la pili. Herrera alipachika bao la tatu na kisha Mesut Ozil kuifungia Arsenal bao la pili na kufanya matokeo kuwa 3-2.
Kinda Marcus Rashford akipiga mpira wa kichwa uliojaa langoni mwa Arsenal
Danny Welbeck akifunga bao lake langoni mwa Manchester United
Nayo Tottenham imekwea pointi mbili nyuma ya vinara wa Ligi Kuu ya Uingereza Leicester City baada ya kupigana kiume kutoka nyuma baada ya kufungwa na kisha kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Swansea.
Mchezaji Alberto Paloschi aliwapatia wageni Swansea bao la kuongoza, huku kabla ya Nacer Chadli kupadili mwelekeo wa shuti la Kyle Walker. Bao la ushindi la Tottenham lilifungwa kwa shuti kali la beki Danny Rose.
Beki wa Tottenham Danny Rose akishangilia bao lake lililoipaushindi timu yake
Tags
MICHEZO KIMATAIFA




