Viongozi
mbalimbali wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA ngazi ya Mkoa
na Taifa hii leo wanatarajia kuzindua Rasmi Ofisi ya Mbunge wa Viti
Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema) iliyopo Mtaa wa Ghana, Kata ya
Nyamanoro Jimboni Ilemela.
Uzinduzi huo utaambana na shughuli mbalimbali ikiwemo kutembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mwanza Sekour Toure. Pichani juu ni Secretary wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Mwanza (Chadema).
Pichani ni Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan Maseke.
Kushoto
ni Ofisi ya Katibu (Mwenye Miwani) wa Mbunge Viti Maalumu Mkoa wa
Mwanza (Chadema) na Kulia ni Ofisi ya Katibu wa Baraza la Wanawake
Chadema (BAWACHA).
Jengo
la Ofisi ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoani Mwanza (Chadema), Susan
Maseke ambayo inatarajiwa kuzinduliwa Rasmi hii leo. Ofisi hii iko
GreenView, Mtaa wa Ghana Kata ya Nyamanoro, Jimbo la Ilemela Mkoani
Mwanza.
Imeandaliwa na George Binagi-GB Pazzo @BMG
Tags
SIASA