Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akifafanua jambo kuhusu ukusanyaji
madeni ambayo Wakala wa Majengo nchini (TBA) inadai wapangaji wake.

Muonekano wa barabara ya
Sakina-Tengeru Km 14.1 inayojengwa kwa njia nne kwa kiwango cha lami ili
kupunguza msongamano wa magari kuingia na kutoka katikati ya jiji la
Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akitoa maelekezo kwa mkandarasi M/S
Hanil Jiangsu J/V anayejenga barabara ya Sakina-Tengeru Km 14.1 na
barabara ya mchepuo wa kusini Arusha bypass Km 42.4 jijini Arusha.

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (kulia) akikagua ripoti ya biashara
inayofanywa na Kampuni ya Simu nchini (TTCL), jijini Arusha. Wa tatu
kulia ni Meneja Kanda ya Kaskazini TTCL Bw. Peter Lusama.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa (katikati) akiimba wimbo wa mshikamano
daima na wajumbe wa Baraza la wafanyakazi wa Wakala wa Barabara nchini
TANROADS kabla ya kufungua rasmi mkutano wa sita wa Baraza hilo. Kulia
ni Mtendaji Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale na kushoto ni Kaimu
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Bw. Fadhili Nkurlu.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisisitiza kufanya kazi kwa malengo
yanayopimika katika kikao chake na wafanyakazi wa taasisi zilizo chini
ya wizara yake, jijini Arusha.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa akisikiliza maelezo ya namna ya
kuhamisha miundombinu ya maji pembeni ya barabara ya Sakina-Tengeru
…………………………………………………………………………………………………………..
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano Prof. Makame Mbarawa ametoa mwezi mmoja kwa makandarasi wote
nchini kuhakikisha wanasaini mikataba ya ajira na wafanyakazi katika
miradi ya ujenzi wa barabara inayoendelea nchini kote.
Akizungumza jijini Arusha mara
baada ya kufanya ukaguzi wa mradi wa ujenzi wa barabara ya
Sakina-Tengeru yenye urefu wa Km 14.1 na barabara ya mchepuo ya kusini
(Arusha bypass) yenye urefu wa Km 42.4, Prof. Mbarawa amesema mkandarasi
atakayeshindwa kutoa mikataba kwa mujibu wa sheria za Tanzania,
atanyang’anywa kazi ya ujenzi kwa kuvunja sheria.
“Barabara zinajengwa kwa kodi za
wananchi hivyo wajenzi wa barabara nao ni lazima wafuate sheria za nchi
ili kuhakikisha Serikali inapata kodi stahili na wafanyakazi wazawa nao
wanapata haki stahili kwa mujibu wa ajira zao”, amesema Waziri Prof.
Mbarawa.
Amezitaka taasisi za TRA, NSSF na
nyingine zinazosimamia ajira za wafanyakazi kufuatilia miradi ya ujenzi
ili kuona fursa za mapato ambazo serikali inaweza kupata na kusajili
wafanyakazi katika hifadhi ya mifuko ya jamii.
Waziri Prof. Mbarawa amewataka
mameneja wa tanroads na maafisa kazi kukagua mikataba ya ajira za ujenzi
katika maeneo yao ili kuona haki inatendeka kwa makandarasi na kwa
wafanyakazi ili ujenzi wa barabara ukamilika kwa wakati na kwa ubora
unaotakiwa.
Katika hatua nyingine Prof.
Mbarawa amefungua mkutano wa Sita wa Baraza la Wafanyakazi la Wakala wa
Barabara nchini (TANROADS) na kuwataka kuweka mikakati itakayowezesha
kulinda hifadhi ya barabara, kudhibiti magari yanayozidisha uzito na
kusimamia kasi katika miradi ya ujenzi wa barabara.
“Mmekua mkifanya kazi nzuri,
endeleeni kufanya kazi kwa uadilifu, uwazi, weledi na kujiwekea malengo
ya kujipima mwaka hadi mwaka ili muendelee kuwa tassisi ambayo watu
watakuja kujifunza kwenu”, amesisitiza Waziri Prof. Mbarawa.
Naye Mtendaji Mkuu wa TANROADS
Eng. Patrick Mfugale amemhakikishia Waziri Mbarawa kuwa TANROADS
imejipanga kuhakikisha miradi ipatayo 90 ya ujenzi wa barabara
inayoendelea nchini kote inakamilika katika ubora unaotakiwa na unao
uwiana na thamani ya fedha.
Aidha, Waziri Prof. Mbarawa
amemuagiza Meneja wa Wakala wa Majengo nchini (TBA), mkoa wa Arusha, Bw.
Victor Baltazar kukusanya madeni yote kwa haraka ili kukamilisha miradi
ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi na za biashara inayosimamiwa na
Wakala huo mjini Arusha kukamilika kwa wakati.
Prof. Mbarawa ambaye yuko katika
ziara ya mikoa ya kanda ya kaskazini amezitaka taasisi zilizo chini wa
wizara hiyo kuhakikisha zinafanya kazi kibiashara ili kuboresha mapato
ya Serikali na hivyo kuiwezesha Serikali kutoa huduma bora kwa wananchi.
Tags
HABARI KITAIFA