NA VICTOR MASANGU, KISARAWE
…………………………………………………
JAMII
hapa nchini imetakiwa kuachana na vitendo vya kuvamia mashamba na
viwanja vya waatu kiholela bila ya kuzingatia na taratibu na
zilizizowekwa kwani kufanya hivyo kunachangia kwa kiasi kikubwa
kuchochea vurugu na na uvunjifu wa amani kutokana na kuwepo kwa migogoro
ya ardhi.
Hayo
yamesemwa na Afisa mtendaji wa Tarafa ya Sungwi iliyopo Wilayani
Kisarawe, Mkoa wa Pwani Thomas Mollel wakati alipokuwa akijibu
malalamiko kwa waandishi wa habari yaliyoyotolewa na baadhi ya wananchi
wa kiluvya ‘B’ kuhusina na suala la uvamizi wa maeneo yao ya viwanja
kinyume na taratibu.
Mollel
alisema kwamba anashangazwa kuona baadhi ya wananchi wamekuwa
wakijichukulia sheria wenyewe kwa kuvamia maeneo ya watu na kuanza
kufanya ujenzi kitu ambacho kimesababisha kuwepo kwa hali ya uvunjifu wa
amani, ambapo ameongeza hawezi kuifumbia macho na atalivaia njuga suala
hio hili haki iweze kutendeka kwa kila mtu mwenye eneo lake kihalali.
“Kwa
kweli mimi sipendi kuoana wanannchi wanavunja sheria ambazo zimewekwa
kwa kuamua kuvamia maeneo ya watu na kuanz akufanya ujenzi hii sio
sahihi kwani kufanya hivyo mwisho wa siku kunaweza kusababisha uvunjifu
wa amani kutokaja na kuibuka kwa migogoro hiyo ya ardhi kwa ahiyo naomba
waachane na tabia hiyo,” aisema Mollel.
Aidha
Afisa Mtendaji huyo alibainisha kwamba wananchi wanapswa kubadiika na
kuzingatia sheria za nchi ziizowewekwa ii kuepekuna na hali ya
kugombania maeneo ya viwanja na mashamba kitu amabcho amedai ni kitendo
cha kujichukulia sheria mikononi.
Kwa
upande wake mmoja wa wananchi ambao wameingia katika mgogoro mkubwa
kutokana na eneo lake kuvamia anayejulikana kwa jina la Januaris Maganga
alimwomba Waziri mwenye dhamana kuliingilia kati sakata hilo kwani kwa
sasa limedumu kwa muda mrefu bila ya kutafutia ufumbuzi jambo ambalo
linamweka katika hali ya kuishi kwa mashaka kutokana na vitisho
anavyovipata kwa sasa.
“Mimi
nina eneo langu kama hekai mbili na nusu lakini nashangaa kuna mzee
mmoja ameamua kulivamia kinyume cha sheria kabisa wakati mimi eneo hii
ni langu kihaai na nina hati ambayo ninayo lakini bado analeta ukorofi
kwa hiyo mimi hai kama hii inabadi waziri mwenye dhamana atusaidie ili
tuweze kutatua mgogoro huu na mimi niweze kupata haki yangu,”alisema
Maganga.
Naye
mmoja wa wazee wa siku nyingi katika kijiji hicho cha kiluvya ‘B;
Rashid Kilusungu akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake kuhusina na
tabia ya wananchi kuvamia maeneo kiholela alisema sio jambo zuri kwani
linaweza kuchochea kutokea kwa vurugu hivyo ni vema busara zikatumika
ili hali ya amani na upendo iwepo.
MIGOGORO
ya viwanja na mashamba katika maeneo ya Wilaya ya Kisarawe bado
inaonekana kuwa ni sugu kutokana na mamlaka ambazo zinahusika
zinachangia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuchelewesha kutoa hati za
wamiliki halali wa maeneo hayo, hali ambayo inasababisha wananchi kuamua
kuvamia na kujenga bila ya kuwa na kibali halali.
Tags
HABARI KITAIFA