DIWANI
wa kata ya Mangaka Halima Mchoma akikabidhi vitabu kwa mmoja wa walimu
wakuu wa shule za msingi nne za kata ya Mangaka hii leo kwenye viwanja
vya shule ya msingi Mangaka.
,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
Na Clarence Chilumba, Masasi
DIWANI wa kata ya Mangaka jimbo la Nanyumbu mkoani Mtwara, Halima Mchoma amenunua vitabu 488 vya masomo ya sayansi na stadi za kazi vyenye thamani ya shilingi milioni 1,157,000/= kwa wanafunzi wa darasa la nne wa shule za msingi za kata hiyo.
Shule zilizonufaika na msaada huo ni pamoja na shule ya msingi Mangaka,Nahawara,Ndwika 2 na Mtokora ambazo zote ni kutoka katika kata ya Mangaka Halmashauri ya Wilaya ya Nanyumbu Mkoani Mtwara.
Vitabu
alivyovinunua diwani huyo ni pamoja na vitabu 388 vya somo la sayansi,
vitabu 100 vya somo la stadi za kazi pamoja na boksi nne za peni zenye
peni 400 ambazo watapewa walimu wa shule za msingi katani humo.
Diwani
huyo ameamua kununua vitabu hivyo pamoja na peni kwa walimu wote wa
kata hiyo kwa fedha zake za mfukoni kwa lengo la kuunga mkono jitihada
za serikali ya awamu ya tano ya kutoa elimu bila malipo.
Akizungumza
leo wakati wa kukabidhi msaada huo kwa walimu wakuu wa shule hizo
katika viwanja vya shule ya msingi Mangaka alisema ameamua kununua
vitabu vingi vya sayansi kutokana na ugunduzi wa gesi mkoani humo ambao
wengi wa wataalamu wanaohitajika ni wale waliosoma masomo ya sayansi.
Alisema
kutokana na kero ya upungufu wa vitabu kwenye kata hiyo waliyokuwa
wanailalamikia walimu ndicho kilichomsukuma kuamua kununua vitabu hivyo
ambapo kwa sasa kila mtoto wa darasa la nne atatumia kitabu kimoja kama
inavyotakiwa kitaalamu.
Mchoma
alisema kwa vitabu vya awamu ya kwanza alivyonunua vina thamani ya
sh.1.2 milioni na kwamba lengo lake kwa sasa ni kutatua changamoto
zilizopo kwenye shule hizo ikiwemo upungufu wa madawati,matundu ya
vyoo,vyumba vya madarasa pamoja na nyumba za walimu.
“Nimeguswa na tatizo la wanafunzi wa kata yangu kutumia kitabu kimoja zaidi ya wanafunzi wawili…ndio maana nimeamua kununua vitabu hivi ambavyo kwa sasa naamini kila mwanafunzi anayesoma darasa la nne kwenye kata hii atatumia kitabu chake na nitafanya hivi kwa kipindi chote cha uongozi wangu ndani ya miaka mitano,”alisema Mchoma.
“Nimeguswa na tatizo la wanafunzi wa kata yangu kutumia kitabu kimoja zaidi ya wanafunzi wawili…ndio maana nimeamua kununua vitabu hivi ambavyo kwa sasa naamini kila mwanafunzi anayesoma darasa la nne kwenye kata hii atatumia kitabu chake na nitafanya hivi kwa kipindi chote cha uongozi wangu ndani ya miaka mitano,”alisema Mchoma.
Alisema
pia amefanya uamuzi huo baada ya kuguswa na namna walimu wa kata hiyo
wanavyojituma katika kufundisha kunakopelekea shule za kata hiyo kufanya
vizuri kwenye matokeo ya mitihani mbalimbali ikiwemo yale ya mtihani wa
kumaliza elimu ya msingi kwa mwaka 2015.
Kwa
upande wake ofisa elimu taaluma wa shule za msingi wilayani Nanyumbu
Stephen Urassa alimpongeza diwani huyo kwa namna alivyoonesha njia na
kwamba msaada huo umekuja wakati muafaka ambao wanafunzi wa darasa la
nne wanajiandaa kufanya mitihani ya majaribio.
“Nimekuwa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu tangu mwaka 2008…lakini sijawahi kuona kiongozi yeyote wa kisiasa akitoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi hivyo hii inaonesha ni kwa namna gani wananchi wa kata ya Mangaka hawakufanya makosa kukuchagua”.alisema Urassa.
“Nimekuwa Halmashauri ya wilaya ya Nanyumbu tangu mwaka 2008…lakini sijawahi kuona kiongozi yeyote wa kisiasa akitoa msaada wa vitabu kwa wanafunzi wa shule za msingi hivyo hii inaonesha ni kwa namna gani wananchi wa kata ya Mangaka hawakufanya makosa kukuchagua”.alisema Urassa.
Naye
mratibu Elimu kata wa kata ya Mangaka Fidelis Hokororo alisema kata
hiyo ina jumla ya wanafunzi 253 wa darasa la nne ambapo kutokana na
msaada huo kwa sasa kila mwanafunzi wa darasa la nne atakuwa anatumia
kitabu kimoja cha sayansi huku vitabu 135 vikiwa zidifu.
Alisema
kwa upande wa vitabu vya stadi za kazi ambavyo ni 100 kwa wastani kila
wanafunzi watatu watakuwa wanatumia kitabu kimoja na kwamba watatumia
baadhi ya vitabu vilivyopo kwenye shule hizo ili kufikia lengo la kila
mwanafunzi kutumia kitabu kimoja.
Tags
ELIMU