BANDA MEDIA BLOG

Klopp amekonga nyoyo za Liverpool, lakini bila kucheza UEFA mwakani ni noma.


33
Manager wa Liverpool ameshindwa nafasi yake ya kwanza kushinda kombe kwenye msimu wake kwanza ndani ya England baada ya kufungwa na Manchester City weekend iliyopita.
Hadi sasa mashabiki wa Liverpool wamefurahishwa na jinsi kocha wao anavyoendesha club hiyo. Lakini changomoto kubwa ambayo ipo kwa Klopp ni kuhakikisha Liverpool inacheza UEFA kwenye msimu ujao.
Wakati anafanya interview ya kwanza kama kocha wa Liverpool Klopp alisema,“Mimi sio aina ya mtu ambae naenda kusema kwamba tutaiteka dunia kwenye soka. Hapana, tutafanya kazi pamoja, tutakua pamoja na kuwa na utaratibu mzuri zaidi ya timu nyingine”
31C50EB900000578-0-image-a-45_1456922156229

Leo Klopp ataiongoza Liverpool ikiwa ni mechi yake ya 19 kwenye EPL tangu awe kocha wa club hiyo. Kwenye rekodi za makocha wa Liverpool ndani ya mechi 18 za kwamza, Klopp yupo namba 3 nyuma ya Rafael Benitez na Kenny Dalglish. Kwenye mechi 18 alizoongoza ameshinda mechi 7, ame-draw mechi 5, amepoteza 6 ambapo anapata uwiano wa asilimia 38.89.

Ndani ya Anfield leo Klopp anategemewa kushinda mechi dhidi ya Manchester City ambayo itakua kama kisasi cha kupoteza mechi dhidi yao kwenye Capital Cup. Kitu cha msingi ni kuendelea kupata points 3 ili waendelee na harakati za kujiweka pazuri na kucheza UEFA msimu ujao.
31C516DF00000578-3472882-image-a-58_1456923639617

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG