Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark
Bi. Agnes Mgongo (katikati) akiongea na waandishi wa habari kuhusu
tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia
litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016, ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa
mgeni rasmi kushoto kwake ni Mratibu wa tamasha hilo Bi. Anawery Phares
na kulia ni mshehereshaji (MC Pilipili) Bw. Emanuel Mathias.
Mratibu wa Tamasha la pamoja la
kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016
Bi. Anawery Phares(katikati) akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari
leo jijini Dar es Salaam kuhusu tamasha hilo ambapo Mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.
Bi. Samia Suluhu Hassan,Kushoto ni Mwanamuzi wa Taarabu Bi. Patricia
Hillary na kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Bi.Agnes Mgongo.
Mchekeshaji na Mshehereshaji Bw.
Emanuel Mathias maarufu kama Mc Pilipili akito kionjo cha mojawapo ya
kichekesho atakachokifanya siku ya tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku
ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5 Machi, 2016,kushoto ni
Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo na kulia ni Mwakilishi wa
Children Survial Hut Tanzania (CSI) Bi.Stella Mranda.
Msanii wa Muziki wa Taarabu
Nchini Bi .Patricia Hillary akieleza jambo wakati wa mkutano na
waandishi wa Habari leo jijini Dar es Salaam kuhusu kwa tamasha la
pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia litakalofanyika tarehe 5
Machi, 2016 ambapo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Mhe. Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi.(Picha na
Lorietha Laurence-Maelezo).
…………………………………………………………………………………………………………………..
Na Beatrice Lyimo-Maelezo
Dar es Salaam,
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Bi. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni
rasmi kwenye Tamasha la pamoja la kuadhimisha Siku ya Wanawake Dunia
litakalofanyika Machi 5, 2016.
Hayo yamesemwa leo jijini Dar es
salaam na Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Agnes Mgongo alipokuwa
akiongea na waandishi wa habari juu ya tamasha hilo ambalo litafanyika
katika ukumbi wa King Solomoni uliopo Nanga jijini Dar es salaam kwa
kujumuisha jinsia zote .
Ameongeza kuwa Kampuni ya Trumark
imeandaa tamasha hilo kwa lengo la kuwahamasisha wanawake kuwa na nguvu
katika nafasi ya kuchangia na kuinua uchumi na maendeleo ya nchini.
“Ni kweli wapo wanawake wenye
mafanikio lakini kuna changamoto zinawakabili ikiwemo uchache wa
ushiriki wa wanaume katika kufanikisha mafanikio ya wanawake na kufungua
fursa ili waweze kuwa sehemu ya mafanikio kwenye sekta mbalimbali za
kiuchumi na kijamii” alifafanua Agnes.
Mbali na hayo Bi. Agnes amesema
kuwa kila mtu kwa nafasi yake ni kiongozi wa kuleta chachu ya maendeleo,
hivyo kila mtu na mahali popote alipo ashiriki vyema kutimiza wajibu
wake huku wakishirikiana na kusaidiana kwa pamoja ili kujenga taifa.
Kwa upande wake mwakilishi kutoka
shirika lisilo la kiserikali linaloshughulika na masuala ya watoto na
wanawake (CSI Tanzania) nchini Stelala Mranda amesema kuwa wameahidi
kuwawezesha wanawake 20 watakaotaka kuhudhuria tamasha hilo.
Wadau mbalimbali wakiwemo Marie
stopes Tanzania, CSI Tanzania, wamejitokeza kudhamini tamasha hilo
lililobeba kauli mbiu isemayo “Pamoja tutafanikisha”.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza
saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa njia za
uzazi wa mpango, upimaji wa saratani ya mlango wa uzazi kwa washiriki
na wananchi wote watakao hudhuria tamasha hilo.
Tamasha hilo linatarajiwa kuanza
saa saba mchana kwa huduma za bure za upimaji na ushauri wa njia za
uzazi wa mpango, upimaji wa saratani ya mlango wa uzazi kwa washiriki
na wananchi wote watakao hudhuria tamasha hilo.
Tags
HABARI KITAIFA