Meneja Mawasiliano
wa Tigo John Wanyancha (Kulia) akiongea na waandishi wa habari (hawapo
pichani) juu ya udhamini wa Tigo wa kiasi cha Shilingi Milioni 11 katika
kampeni ya ‘KUTOA AHADI YA UWIANO WA KIJINSIA ambayo inatarajiwa
kuanza na matembezi ya kilomita 6 ambayo yataanzia kwenye “Uwanja wa
Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5 saa 12 asubuhi,
katikati Mwenyekiti wa Taasisi ya TANZANIA WOMEN OF ACHIEVEMENT
(TWA), Sadaka Gandi na kushoto ni Rais wa (TWA,) Irene Kiwia ambao
ndio waandaaji wa matembezi hayo, kwenye mkutano uliofanyika mapema leo
jijini Dar es salaam.
………………………………………………………………………………………….
Kampuni
ya Tigo Tanzania imedhamini kampeni ya Kutaka Uwiano ambayo
inatarajiwa kuanza na matembezi ya kilomita sita ambayo yataanzia
kwenye “Uwanja wa Mbio za Mbuzi”, Masaki, Dar es Salaam Jumamosi Machi 5, 2016.
Kampeni hiyo imeandaliwa na Taasisi ya Wanawake wenye Mafanikio (TWA) ambayo ni asasi isiyo ya kiserikali
ambayo lengo lake kuu ni kuimarisha ushiriki, na majukumu yawanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mambo ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
ambayo lengo lake kuu ni kuimarisha ushiriki, na majukumu yawanawake na uwezo wao katika jamii ya Tanzania kwenye mambo ya kijamii, kisiasa na kiutamaduni.
Kutoa
Ahadi ya Uwiano wa kijinsia ni kauli mbiu ya mwaka huu katika
Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wanawake. Ambayo kilele
chake kitakuwa Machi 8, 2016.Kampeni ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa jinsia
inatoa wito kwa kila mtu kuchukua hatua za dhati kusaidia upatikanaji wa
uwiano wa kijinsia kwa kasi zaidi ilikuwa saidia wanawake na wasichana
kufikia matamanio yao.
Matembezi hayo ya tafuatiwa na Kongamano la Siku ya Kimataifa ya Wanawake litakaofanyika kwenye Hoteli ya
Regency Kilimanjaro, Jumapili, Machi 6. Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kwamba kama kampuni ya maisha ya kidijitali Tigo inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wanawake ndani ya jamii na ndio maana kampuni hiyo inaungana na watu wenye mapenzi mema kuunga mkono kampeni ya TWA.
Regency Kilimanjaro, Jumapili, Machi 6. Akizungumza kwenye mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Meneja Mawasiliano wa Tigo, John Wanyancha alisema kwamba kama kampuni ya maisha ya kidijitali Tigo inatambua mchango mkubwa unaotolewa na wanawake ndani ya jamii na ndio maana kampuni hiyo inaungana na watu wenye mapenzi mema kuunga mkono kampeni ya TWA.
“Tigo
inajivunia kuunga mkono TWA kwenye kampeni hii ambayo ambayo inatafuta
kuwawezesha wanawake kuingia kwenyeustawi wa wasaidie wengine kustawi
kwa ajili ya manufaa ya jamii. Ikiwa ni kampuni inayoendeshwa
kwa ubunifu, Tigo iko tayari kufanya kazi na watu wengine ambao ni
wabunifu, jamii, asasi zisizo za serikali, serikali, sekta binafsi na za
umma kwa ajili ya manufaa ya jamii yote,” alisema Wanyancha.
Akitoa
shukrani zake kutokana na kuungwa mkono huko,Rais wa TWA, Irene Kiwia
aliishukuru Tigo kutokana na kujikita kwake kusaidia mikakati mbalimbali
ambayo imejielekeza katika kuisaidia jamii.
Kiwiaalisema,
“Wakati tunakaribia kuanza Kampeni ya Kutoa Ahadi ya Uwiano wa
kijinsia,tunapenda kuishukuru Tigo kwa ukarimu wake wa kutuunga mkono.
Bila
uungwaji mkono wa kampuni hii pamoja na huduma zake kubwa hatungeweza
kufikia malengo yetu mengi katikakupanga na kuandaa kampeni hii.
Uungwaji mkono wa Tigo utakuwa na matokeo ya muda
mrefu yatakayowanufaisha wanawake kufuatia mafanikio ya kampeni hii.”
Hali
kadhalika Kiwia alitoa wito kwa watu kushiriki kwenye Matembezi ya
Kutoa Ahadi ya Uwiano wa kjiinsia akisema, “Tunatoa wito kwa watu
binafsi, asasi zisizo za serikali, vyombo vya habari, maofisa wa sekta
za umma na binafsi na wadau wengine kuja kwa wingi na kuungana na
sikushiriki kwenye matembezi na waalikwa kushiriki kwenye Mkutano wa
Siku ya Kimataifa ya Wanawake.
rasmi katika matembezi hayo. Licha ya kutoa suluhisho la kiteknolojia kidijitali la kisasa hapa nchini, Tigo kwa miaka mingi imekuwa ikisaidia mikakati ya kijamii ambayo yanaleta manufaa makubwa kwa jamii
Tags
HABARI KITAIFA



