Polisi watatu wa wilayani Urambo, Mkoa wa Tabora wamefikishwa mahakamani kwa mashitaka ya kuomba na kupokea rushwa.
Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) mkoani Tabora, iliwafikisha
askari hao jana katika Mahakama ya Wilaya ya Urambo huku mwingine
akidaiwa kukimbia.
Askari hao waliofukuzwa kazi kabla ya kufikishwa mahakamani ni John Okinda, Kabila Pius na Patrick Robart.
Anayedaiwa kukimbia ni Elisha ambaye polisi inaendelea kumtafuta.
Mbele ya Hakimu
Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya wilaya ya Urambo, Hassan Momba, Wakili wa
Takukuru, Edsoni Mapalala alidai washitakiwa walitenda makosa hayo
Machi 7 mwaka huu.
Mapalala alidai
siku hiyo katika kijiji cha Mkirigi, Kata ya Ilege, Wilaya ya Kaliua,
washitakiwa hao wakiwa waajiriwa wa jeshi la polisi, waliomba rushwa ya
Sh milioni tatu kutoka kwa Dotto Gandulanye ili wasimchukulie hatua za
kisheria baada ya kumkuta akiwa na bangi.
Tags
HABARI KITAIFA
