BANDA MEDIA BLOG

Waziri Profesa Makame Atembelea daraja la Nyerere na Kituo cha kupimia mafuta yaingiayo nchini kuona Maendeleo

p1Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akiongea na wawakilishi wa kampuni ya Mabey Bridge kutoka Marekani(hawapo pichani) na wadau wengine wa Ujenzi leo kuhusu mpango wa kujenga fly overs takribani tatu katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji.
p2Katibu mkuu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Sekta ya Ujenzi) Eng. Joseph Nyamhanga akifafanua jambo kuhusu mpango wa ujenzi wa kujenga fly overs katika jiji la Dar es salaamu kwa lengo la kupunguza msongamano wa magari katika jiji hilo kushoto ni muakilishi kutoka Kampuni ya Kimarekani ya Mabey Bridge Bw. Darren Keep na kulia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.
p3Msimamizi Mkuu wa Daraja la Nyerere Bw. Gerald Sondo akieleza jambo kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa kuhusu maendeleo ya Daraja pamoja na changamoto wanazozikabili, katika Ziara ya kushtukiza iliyofanya na Waziri huyo leo jijini Dar es salaamu.

p4
p5 p6Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa Fundi mitambo Bw. Simon Dotto  kuhusu maendeleo ya ukarabati wa mtambo wa kupima mafuta kutoka kwenye meli kabla ya kuingia kwenye matanki ambao uliharibika hivi karibu kutokana na mvua iliyoambatana na upepo mkali.
p7 p8Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo  kutoka kwa mmoja wa wahudumu wa kivuko cha Mv Magogoni kuhusu utaratibu wa ukatishaji tiketi katika kivuko hicho leo jijini Dar es Salaam.
p9Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akipata maelezo na changamoto mbalimbali kutoka kwa abiria wanaotumia kivuko cha Mv Magogoni leo jijini Dar es Salaam.
(Picha zote na Beatrice Lyimo)

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG