Rais wa Shirikisho la soka nchini, Jamal Malinzi akimkabidhi Kombe la
Ubingwa wa Shirikisho (ASFC), Nahodha wa Timu ya Yanga, Nadir Haroub,
mara baada ya kutwaa ubingwa huo kwa kuichapa Timu ya Azam FC, Bao 3-1,
katika mchezo uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa jijini, Dar
es salaam.
Wachezaji
wa Timu ya Yanga pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kutwaa
Kombe la Shirikisho, kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam leo.
Picha kwa hisani ya Michuziblog.