Na Mwandishi Wetu, Mkuranga
NAHODHA wa Timu ya Soka ya Tanzania (Taifa Stars) Mbwana Ali
Samatta ameahidi kujenga kituo maalum nchini cha kuibua na kukuza
vipaji vya wanasoka wachanga ili wafikie viwango vya kimataifa.
Sambamba na hilo, ameweka azma ya kukifanya kituo chake kuwa na wigo mpana wa kuwawezesha vijana wa kutoka nje ya Tanzania kuja kujifunza soka katika kituo hicho na kuwapeleka vijana wawili kila mwaka kwenda kujifunza zaidi mchezo huonchini Ubelgiji.
Hayo yamebainishwa na baba wa mwanasoka huyo wa kimataifa, Ali Samtta alipozungumza kwa niaba ya mwanae, katika halfa ya kukabidhiwa ekari tano za eneo la ujenzi wa kituo hicho kulikofanywa na Mtandao wa Wasanii na Wanamichezo nchini, (SHIWATA.)
Hafla ya makabidhiano hayo yaliyofanyika juzi katika kijiji cha wasanii kilichopo Mwenzanga, wilayani Mkuranga.
Akizungumza kwa niaba ya mwanae, baba wa nyota huyo alisema, azma ya Samatta (Mbwana) ni kujenga kituo kikibwa cha kimataifa ambacho, moja ya madhumuni ni kuendelea kuwaibua na kuwakuza akina ‘Samatta’ wengine wajao.

“Niliongea na Mbwana amenituma niwakilishe salamu zake kwa kwanza kwa kuishukuru SHIWATA na kisha kueleza nia yake ya kutaka kuendelea kuibua vipaji vya soka la vijana kupitia kituo kitakachojengwa hapa katika kijiji cha wasanii Mwenzange” alisema Ali Samatta na kuongeza.
“Engekuwapo hapa leo, lakini alilazimika kusafiri mara tu baada ya kumalizika kwa mechi ya Stars dhidi ya Misri, kurejea Ubelgiji kwa wito wa haraka, lakini anatarajia kurejea tena nchini kwa mapumziko, na mimi amenituma nimwakilishe kwa kauli zake hizi”
Katika hatua nyingine, mwakilishi wa mgeni rasmi, Nape Mnauye, Bi
Leah Kihindi aliipongeza SHIWATA kwa hatua yake ya kuwawekea misingi
wanachama wake ili wawe na makazi ya kudumu kupitia kijiji hicho.
Sambamba na hilo, alilipongeza shirikisho hilo kwa kutambua mchango wa Mbwana Samatta katika soka ambako katika sherehe hizo wanachama 35 walikabidhiwa nyumba na misingi ya kujenga nyumba.
Mwenyekiti
wa SHIWATA Cassim Taalib akiwatoa taarifa fupi ya kijiji hicho alisema
lengo ni kuwasaidia wasanii, wanamichezo na waandishi wa habari kujenga
nyumba za kuishi ili kujiandaa kwa ajili ya kuishi maisha ya taabu baada
ya kustaafu kazi zao.
SHIWATA inayomiliki ekari 300 za makazi katika kijiji hicho jumla ya wanachama 185 wamnejenga nyumba kwa njia ya kuchangishana.
Sambamba na hilo, alilipongeza shirikisho hilo kwa kutambua mchango wa Mbwana Samatta katika soka ambako katika sherehe hizo wanachama 35 walikabidhiwa nyumba na misingi ya kujenga nyumba.
SHIWATA inayomiliki ekari 300 za makazi katika kijiji hicho jumla ya wanachama 185 wamnejenga nyumba kwa njia ya kuchangishana.
Tags
MICHEZO KITAIFA