Mmoja wa
wachezaji maarufu wa soka barani Afrika Stephen Keshi amefariki akiwa na
umri wa miaka 54 ,shirikisho la Nigeria limethibitisha.
Nahodha huyo wa
zamani wa kikosi cha Nigeria, Keshi,alikuwa mmoja wa watu wawili pekee
kushinda michuano ya kombe la bara Afrika akiwa mchezaji na kocha.
Pia alifunza
Togo na Mali,na aliwahi kuichezea timu ya Anderlecht ya
Ubelgiji.Anadaiwa kuugua mshtuko wa moyo,kulingana na vyombo vya habari
vya taifa hilo.
Akiwa mchezaji
,keshi alikuwa katika kikosi cha Super Eagles kilichoshinda kombe la
bara Afrika mnamo mwaka 1994 na kushindwa kushirki katika mechi za robo
fainali za kombe la dunia mwaka huohuo.
Alikuwa
mkufunzi wa kikosi cha Nigeria kwa vipindi vitatu ,na kuisaidia Nigeria
kufuzu katika michuano ya bara Afrika 2013 nchini Afrika Kusini pamoja
na kombe la dunia mwaka 2014 huko Brazil.
via bbcswahili.com
Tags
MICHEZO KIMATAIFA
