Shirika la
Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) limekosoa vikali hali
mbaya inayowakabili wakimbizi watoto nchini Ujerumani na kusema kuwa
hawapewi huduma zinazofaa za tiba wala elimu.
Ripoti ya
UNICEF imesema kuwa, wakimbizi watoto nchini Ujerumani hawapewi huduma
ya elimu kwa miezi kadhaa sasa. Imeongeza kuwa vijana wanahitaji
usimamizi na ulinzi bora zaidi kutokana na unyanyasaji wanaukumbana nao
katika kambi kubwa na kwamba wakimbizi watoto waliopatwa na matatizo ya
kinafsi kutokana na mashaka ya vita, wanahitaji huduma maalumu kama za
wenzao wa Ujerumani.
Mkuu wa ofisi
ya UNICEF nchini Ujerumani, Christian Schneider amesema watoto wote wana
haki sawa bila ya kujali wanatoka wapi au ni wa jamii ipi.
Awali Shirika
hilo la Watoto la Umoja wa Mataifa lilikuwa tayari limetahadharisha kuwa
wakimbizi watoto wanalazimishwa kutenda uhalifu au kujihusisha na
ukahaba nchini Ufaransa.
Tags
KIMATAIFA
