BANDA MEDIA BLOG

DC HASHIMU ATOA TAHADHARI HII KWA WAKAZI WA KIGAMBONI



MOSHI SHABANI MALLEMA

Tanzania ni moja ya nchi pekee Duniani iliyofanikiwa kuilinda na kuitunza Amani yake iliyoasisiwa na viongozi wake wakuu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Amani Abeid Karume, hivyo kwa kwakuzingatia hayo Mkuu wa Wilaya mpya ya Kigamboni Hashimu Shaibu Mgandilwa ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama, amezungumza na wanakigamboni kuhusu Amani hiyo na kutoa tahadhari.DC HASHIMU KIGAMBONI TAHADHARI (6)

Ambapo ameeleza kuwa hivi karibuni wamejitokeza watu wachache wasio litakia mema taifa la Tanzania kwa maslahi yao binafsi na kuona amani iliyopo haina thamani wakiwashawishi watu kuandamana wakati familia zao wame zisafirisha kwenda nje ya nchi.DC HASHIMU KIGAMBONI TAHADHARI (1)

Hivyo Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni na akiwa kama Mwenyekiti wa Ulinzi na Usalama katika Wilaya yake amewaomba wananchi wa Kigamboni vijana kwa wazee, wanawake kwa wanaume na makundi yote ya kijamii katika wilaya yake kuendelea kuilinda na kuitunza Amani ya nchi, kama ilivyo asisiwa na viongozi waanzilishi wa Taifa hili mpaka hii leo wanafurahia maisha yao yenye utulivu.DC HASHIMU KIGAMBONI TAHADHARI (4)

 Huku akiwaasa Wanakigamboni wote kwa kuwataka kutokushiriki katika vitendo vya aina yeyote vyenye mlengo wa kuvuruga Amani, ikiwemo maandamano yasiyo na tija kwa taifa na maisha ya watanzania.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG