August 3 2016 Umoja wa vijana chama cha ACT-Wazalendo
umekutana na waandishiwa habari Dar es salaam na kuzungumzia changamoto
zilizopo katika sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja kitendo
kilichofanywa na serikali kwa kuwasimamisha masomo wanafunzi wa Chuo
kikuu Dodoma (UDOM) wasiokuwa na sifa na baadae kuwarudisha baadhi yao.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao Kitentya Luth ambaye ni mratibu wa vijana ACT-Wazalendo amesema…>>>‘Katika
uamuzi huo wa kuwafukuza watoto wa kimaskini kutoka UDOM kukaibuliwa
lugha za udhalilishaji kwa kuwaita Vilaza bila kuangalia athari za
kisaikolojia‘
‘Sisi kwa nafasi
yetu kama vijana tunalaani vikali udhalilishaji huo mbali ya kulaani
tunaitaka Serikali ituambie na kutujibu masuala matatu yakiwemo‘ –Kitentya Luth
- Je, ni kweli tatizo lilikuwa Udahili ambao haukukidhi vigezo au ni ukosefu wa fedha baada ya wafadhili kujitoa kama tunavyosikia?
- Mliwezaje kuwapata wanafunzi zaidi ya 300 mkidai wamekidhi vigezo vya kurudi chuo na tunafahamu 7000 walikosa sifa kwa matokeo yao kuwekwa hadharani?
- Serikali imewapeleka wanafunzi katika vyuo vingine, je, waliopelekwa walienda kuendelea na elimu waliyoanza awali au walikuwa na mwanzo mwingine
Tags
SIASA