BANDA MEDIA BLOG

USAJILI WA POGBA KWENDA MAN UNITED ULIVYOVUNJA REKODI 5 ZA REAL MADRID


Paul Pogba 1
Manchester United imethibitisha kukamilisha uhamisho wa kiungo wa Juventus Paul Pogba ambaye amejiunga na mashetani wekundu wa ada iliyoweka rekodi ya dunia, kwa mujibu wa tovuti rasmi ya Manchester United.
Baada ya uvumi na tetesi za muda mrefu, miamba hiyo ya EPL hatimaye siku ya Jumapili waliujulisha ulimwengu kwamba, dili la mfaransa huyo kurejea Old Trafford linakaribia kukamilika baada ya kuanza  kwa mchakato wa kumfanyia vipimo vya afya.
Alfajiri ya Jumanne, United wali-tweet kwamba, mchezaji huyo wa zamani wa klabu hiyo amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia klabu hiyo wenye kipengele cha kuongeza mwaka mmoja zaidi.
Uhamisho huo unatajwa kugharimu £89m, ukivunja rekodi ya ya usajili ghali zaidi duniani wa £85m uliomshuhudia Gareth Bale akihama kutoka Tottenham Hotspur na kujiunga na Real Madrid mwaka 2013.
Usajili wa Paul Pogba umevunja rekodi ya sajili tano ghali zaidi duniani katika miaka ya hivi karibuni ambapo wachezaji wote walihamia vilabu vya La Liga, (Hispania).
Ikumbukwe wachezaji wote hao watano walikuwa wakitoka vilabu vinggine wakihamia Real Madrid. Kwahiyo tangu mwaka 2000-2013, Real Madrid pekee ndiyo klabu iliyosajili wachezaji kwa dau kubwa zaidi duniani rekodi ambayo imevunjwa na Manchester United mwaka 2016.
2000 – Luis Figo £37m (Barcelona to Real Madrid)

Usajili 1

2001 – Zinedine Zidane £46m (Juventus to Real Madrid)
MADRID, SPAIN - JULY 9:  French soccer star Zinedine Zidane displays his new Real Madrid soccer club jersey during the presentation of Zidane as the new team player in Madrid on Monday 09 July 2001.  (Photo credit should read MARC ALEX/AFP/Getty Images)
2009 – Kaka £56m (AC Milan to Real Madrid)
Usajili
2009 – Cristiano Ronaldo £80m (Manchester United to Real Madrid)
Usajili 3
2013 – Gareth Bale £86m (Tottenham Hotspur to Real Madrid)
Usajili 4

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG