Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema (pili kulia) akiwa sambamba na
Katibu Tawala wa wilaya hiyo Edward Mpogolo (tatu kushoto) wakishiriki
mazoezi ya pamoja ya kikundi cha klabu ya Mazoezi cha New Life
Jogging,na vikundi vingine mbalimbali vya mazoezi , mapema leo asubuhi
katika viwanja vya Kimanga,Tabata Mawenzi,jijini Dar,ambapo Mkuu wa
Wilaya alialikwa kuwa mgeni rasmi kwenye hafla fupi ya kikundi cha New
Life Jogging kilipokuwa kinatimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa
kwake.PICHA NA MICHUZI JR-MMG.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akikabidhiwa Risala na Mwenyekiti wa
kikundi cha Newa Life Jogging,Baraka Urio akiwa ameambatana na
wanachama wa kikundi hicho,mara baada ya kuisoma na kuelezea changamoto
na fursa mbalimbali zilizopo ndani ya kikundi hicho.Kikundi hicho chenye
makazi yake Tabata Mawenzi leo kimetimiza mwaka mmoja tangu kuanzishwa
kwake.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akizungumza mbele ya vikundi
mbalimbali vya mazoezi (havipo pichani),vilivyoshiriki kwenye hafla hiyo
fupi ya kutimizwa mwaka mmoja wa kikundi cha New Life Jogging.Mh.Mjema
aliwataka viongozi wa vikundi hivyo kuelezea changamoto zao walizo nazo
ikiwemo na fursa zilizopo ili serikali kupitia Ofisi yake ziweze
kufanyiwa kazi kwa wakati.Mh Mjema alisema kuwa Jogging sio
uhuni,isipokuwa kuna watu walitaka kupenyeza mambo yao katika Jogging.
“Lakini
wale waliotaka kuyapenyeza hayo,waliotaka kuingiza uhalifu,waliotaka
kupenyeza madawa ya kulevya ,waliotaka kuingiza siasa,waliotaka kuingiza
Panya rodi washindwe na walegee,hatutaki Jogging zetu
zichafuke,tunataka Jogging zitumike kuona fursa zilizopo”,alisema Mh
Mjema.
Katibu
Tawala wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo akiwasalimia na kuwatia
moyo vikundi hivyo vya Jogging,ambaye pia aliwaeleza kuwa wakati wa
kujituna na kufanya kazi ni sasa,hivyo amewaomba viongozi wa vikundi
hivyo kukutana nao ili kuhakikisha fursa na changamoto walizozieleza
katika risala yao zinafanyiwa kazi kwa wakati.
Mkuu
wa wilaya ya Ilala Mh Sophia Mjema akikabidhiwa jezi na Mwenyekiti wa
kikundi cha New Life Jogging,Baraka Urio,pichani kati ni Katibu Tawala
wilaya ya Ilala,Ndugu Edward Mpogolo na wadau wengine wakishuhudia tukio
hilo.
Mgeni
rasmi,Mkuu wa Wilaya ya Ilala Mh.Sophia Mjema na viongozi wengine
waandamizi kutoka ofisi ya Mkuu wa wilaya wakiwa katika picha ya pamoja
na Kikundi cha New Life Jogging,ambacho leo kinasherehekea kutimiza
mwaka mmoja tangu kuanzishwa kwake.
Vikundi mbalimbali vilishiriki kwenye mazoezi hayo ya pamoja.
Tags
MICHEZO KITAIFA