Na Athumani Adam
Stars na Nigeria zinakutana kwa mara ya nane kwenye mchezo wa mwisho wa kuwania kufuzu Afcon 2017. Japokuwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba baada ya timu ya Misri kuwa tayari imefuzu kutoka kwenye Kundi G, lakini Stars inatafuta rekodi kwa kuifunga Nigeria kwa mara ya kwanza katika ngazi ya timu za wakubwa.
Kabla ya mechi ya leo Stars na Nigeria zimekutana mara saba (7), Nigeria imeshinda mara nne (4) na kutoka sare mechi tatu (3). Makala hii inakupa kumbukumbu ya mechi zote saba baina ya mataifa haya
- Nigeria 1 – 1 Tanzania, FIFA World Cup Qualifier (6 December 1980)
Kikosi cha stars kilikuwa: Juma Pondamali, Thuwein Ally (sub Kajole), Ahmedi Amasha, Yusufu Bana, Charles Boniface, Omar Hussein(sub Peter Tino) , Juma Mkambi, Jella Mtagwa, Mohammed Rishard, Mohammed Salim, Leodger Tenga
- Tanzania 0 – 2 Nigeria, World Cup Qualifier (20 December 1980)
Kikosi cha stars kilikuwa: Juma Pondamali, Thuwein Ally, Yusufu Bana ( sub Mohamed Rishrad), Isihaka Hassan, Omar Hussein, Mohamed Kajole, Juma Mkambi, Jela Mtagwa, Hussein Ngulungu (sub Charles Boniface), Mohammed Salim, Peter Tino
- Nigeria 3 – 1 Tanzania, Africa Cup of Nation (8/3/1980)
Kwenye mashindano hayo Tanzania ilipoteza mchezo dhidi ya Nigeria ambayo ilikuwa ni mechi ya ufunguzi. Pia Tanzania ilipoteza tena dhidi ya Misri 2-1 na kutoka sare dhidi ya Ivory Coast kwenye mechi ya mwisho.
Kwenye mechi dhidi ya Nigeria kikosi cha Tanzania kilikuwa: Othumani Mambosasa, Mohamedi Kajole, Jela Mtagwa, Ledger Tenga, Tasso Mukebezi, Omar Hussein, Juma Mkambi(mfungaji wa bao), Ngulungu, Massewa, Ramadhani, Waziri (sub Peter Tino)
- Nigeria 2 – 1 Tanzania, All Africa game (12 January 1973)
Kwenye mashindano haya Tanzania ilifanikiwa kupata medali moja ya dhahabu baada ya mwanariadha Filbert Bayi kushinda mbio za mita 1500.
- Tanzania 0 – 0 Nigeria, Afcon Qualifer (5/9/2015)
Bahati mbaya Tanzania haikufanikiwa kufunga bao hata moja na hatimate mechi ikamalizika kwa sare.
- Tanzania 0 – 0 Nigeria, International friendly (6 June 1972)
- Nigeria 2– 0 Tanzania, International friendly (11 September 2002)
Tags
MICHEZO KIMATAIFA