Kituo cha TV cha Azam TV kimeripoti kwamba September 3 2016 Rais
Magufuli akiwa kwenye ziara yake visiwani Zanzibar ametoa hotuba ambapo
amemshauri Rais wa Zanzibar kuwa mkali zaidi huku akizungumia tukio la
Katibu mkuu wa CUF Maalim Seif kukataa mkono wa Rais Shein wakati
akimsalimia.
’Kama mtu anaukataa mkono wako na wewe kataa mkono wako kufanya mambo
yake, ajifunze ajue mkono wako una thamani, haiwezekani mbele ya watu
unashike mkono anakataa halafu unatoka ofisini unasema unasaini hapa
hela ya huyu kwenda kutibiwa’:-JPM