Kongamano kwa ajili ya kujadili matatizo na maendeleo ya soka la Tanzania ambalo linafanyika kwa siku mbili jijini Dar es Salaam, limeanza leo katika uwanja wa taifa chini ya maandalizi ya Jukwaa la Kandanda
Jukwaa hilo limelenga katika kuimarisha misingi ya uendeshaji ya mchezo wa mpira wa miguu, leo ilikuwa ni siku ya kwanza ambapo limekuwa likitangazwa kwa muda wa juma zima, mambo mengi yamejadiliwa katika siku ya kwanza ikiwemo kufamu namna gani ya kuendesha vilabu vya soka pamoja na mpira wa miguu.
Kulikuwa na fursa kubwa ya kufahamu kuhusu leseni za vilabu na jinsi soka la Tanzania linavyoweza kuathirika endapo leseni za vilabu hazitokamilika hususan kwa vilabu ambavyo vinashiriki michuano ya kimataifa.
Jambo ambalo si lakupenda ni pale viongozi wa vilabu vya soka hasa vile vya ngazi za juu kushindwa kujitokeza kwenye jukwaa hilo kusikiliza au kujua ni kitu gani kinafanyika kwenye chukwaa hili.
Hata rais wa TFF Jamal Mlinzi hakuonekana kwenye jukwaa hilo huku kukiwa hakuna sababu iliyotolewa wakati kwenye ratiba jina lake lilikuwepo.
“Mimi nafikiri kikubwa ambacho kimeandaliwa kwa mara ya kwanza, tungependa iwe bora zaidi lakini bado tunaona kunamafanikio kwasababu tumepata watu kama 35 huku kukiwa na waandishi wa habari wa kutosha ambapo tunafikiri vitafikisha ujumbe kwa jamii”, amesema Henry Tandau mmoja wa waraibu wa kongamano hilo lakini pia alikuwa ndiyo mtoa mada.
Kuhusu kukosekana kwa viongozi muhimu wa vilabu Tandau alisema: “Mimi nafikiri hayo ni matatizo ya Tanzania kwa ujumla watu wengi katika Nyanja nyingi huwa hawako tayari kupewa mawazo au michango ya taamula, sasa hilo ni tatizo lakini sisi tuko hapa kutoa elimu siyo kwa vilabu tu bali kwa wote wanaojihusisha na mpira wa miguu.”
Kongamano hilo litaendelea tena kesho September 4 ambapo ndiyo itakuwa kilele chake
Tags
MICHEZO KITAIFA