Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo
October 24 2016 amefanya mazungumzo na mgeni wake Mtukufu Mfalme wa
Morocco Mohamed VI.
Ziara ya
mfalme huyo ni kuimarisha uhusiano baina ya Morocco na Tanzania, mfalme
Mohamed VI akiwa Ikulu Dar es salaam na ujumbe wake wamesaini
makubaliano takribani 22 ya ushirikiano katika sekta ya kilimo, gesi,
mafuta, reli ya Liganga na Mchuchuma na Sekta ya utalii.
Baada
ya kutiliana saini kwa mikataba ya makubaliano ya ushirikiano kati ya
nchi za Tanzania na Morocco Rais Magufuli amesema kuwa wamekubaliana na
Mfalme Mohamed VI wa Morocco kujenga Uwanja wa Mpira wa miguu wa kisasa
mkoani Dodoma utakaogharimu dola milioni 100.
>>>’Mbali
na mikataba baina ya Tanzania na Morocco nimezungumza mambo
mbalimbali na Mfalme Mohamed VI wa Morocco na nimemuomba atujengee
Uwanja mkubwa wa mpira pale Makao Makuu yetu Dodoma utakaokuwa na
thamani kati ya dola milioni 80 hadi 100 na amesema ataujenga, kwa hiyo
utakuwa Uwanja mkubwa kuliko wa Dar es Salaam‘.
Unaweza kuangalia video hii hapa chini
Tags
BIASHARA