Na Rashid Seif
“Hii ndio October mosi 2016, YANGA VS SIMBA imeacha historia, maswali, kumbukumbu, ndio hii October mosi nchi ilikuwa kwenye upandaji miti, hii ndio October mosi ya Yanga na Simba, October mosi ya Martin Saanya, Hii ndio Octoba mosi Pope Damasmus 1 alipochaguliwa pale Rome mwaka 366, October Mosi Edgar the Peaceful alikuwa mfalme wa England yote mwaka 959, hii ndio October mosi ya THRILLA MANILA gwiji wa masumbwi (Marehemu) Muhammad Ali alimpiga Joe Frazier. Kama (nilivyosema) kwenye makala iliyopita ya dondoo na uchambuzi kuelekea Octoba mosi YANGA vs SIMBA.
Leo nitakuchambulia tena.
UCHAMBUZI WA KINA (TACTICAL ANALYSIS):
UTEUZI WA VIKOSI (SQUAD SELECTION)
YANGA:
LINDA MLANGO: Ally Mustafa ‘Barthez’
MABEKI: Juma Abduli, Vicent Bossou, Kelvin Yondani (Vincent Andrew), Haji Mwinyi
VIUNGO: Mbuyu Twite, Juma Mahadhi (Simon Msuva), Thaban Kamusoko, Deus Kaseke (Haruna Niyonzima).
WASHAMBULIAJI: Donald Ngoma, Amissi Tambwe
MFUMO: 4-4-2
Yanga ilifanya mabadiliko mawili kutoka kwenye kikosi kilichpita kilichocheza dhidi ya Stand United. Kelvin Yondani alianza badala ya Vicent Andrew, hii ni kwa sababu Kelvin ni mzoefu wa hii mechi ya watani wa jadi alianza kucheza tokea alipokuwa Simba na sasa yupo Yanga anajua ugumu wa mechi hii.
Wakati Juma Mahadhi alianza badala Msuva kwa sababu hawa wote ni wazuri, utofauti wao upo katika baadhi ya vitu Msuva ni mkimbiaji sana (runner), Juma Mahadhi ni mkimbiaji (runner) na pia anauwezo wa kukaa na mpira (ball holder), mpigaji mzuri wa pasi (good passer), mpigaji mzuri wa mashuti ya mbali kwenye mechi kama hii unahitaji mchezaji ambaye atatoa alichonacho baada ya mbinu za mwalimu kukwama mfano goli lake dhidi African Lyon haya ndio aliyomzidi Simon Msuva, Kwa aina ya mechi ya Simba na Yanga unahitaji wachezaji kama hawa ball holders hawa kazi yao kubwa kupunguza presha ya mechi “game tempo” hii ndio ilikuwa kazi ya Juma Mahadhi ndio maana Simba pamoja na kuanza kwa kasi YANGA walifanya kazi ya kupunguza presha wakisaidiwa na mlinda mlango wa simba Vincent angban.
Nilishangazwa kwanini sikumuona Deogratius Munishi golini pia nafikiri lilikuwa kosa la mwalimu yanga ‘Dida’ ni mziefu amecheza mechi za kimataifa za Yanga kwa game kama Simba na Yanga Dida alikuwa na nafasi kiuzoefu na kiwango
SIMBA:
MLINDA MLANGO: Vincent Angban
MABEKI: Janvier Bokungu, Method Mwanjali, Novert Lufunga (Juko Murshid), Mohammed Hussein “Tshabalala”.
VIUNGO: Shiza Kichuya, Jonas Mkude, Muzamir Yassin, Mwinyi Kazimoto.
WASHAMBULIAJI: Ibrahim Ajib (Ibrahim Mohammed), Laudit Mavugo (Fredrick Blagnon).
MFUMO: 4-4-2
Simba walifanya mabadiliko mawali kutoka kwenye kikosi kilichopita kwenye mechi dhidi Majimaji, Novert Lufunga badala ya Juuko Murshid, hili ni moja ya kosa alilolifanya Mwalim Omog na lilimgharimu sana, Niliongea (kwenye makala iliyopita) uelewano uliopo baina ya Method Mwanjali na Juko Murshid, bila shaka wengi walitegemea hawa wawili wangeanza mbele ya golikipa Vincent Angban, Ilikuwaje Omog kumuacha beki tegemezi wa timu ya taifa ya Uganda atakayeenda kucheza mataifa ya Afrika.
Novert Lufunga alifanya makosa mengi goli la Amissi Tambwe ni ukabaji wake mbovu (poor marking), rafu zisizokuwa na msingi (kama ile aliyomfanyia Juma Abduli),haikushangaza Novert Lufunga kutolewa na nafasi yake kuchukuliwa na Juuko Murshid. Pia Mwinyi Kazimoto badala ya Jamal Mnyate, hili ni badiliko la kimbinu zaidi, Jamal Mnyate ni kiungo mshambuliaji au winga “inverted winger”, Mwinyi Kazimoto ni kiungo hapa mwalimu alihitaji kuhakikisha wanamiliki mpira hivyo alihitaji mtu ambaye angeweza kuhakikisha wana-win midfield battle.
Mwinyi Kazimoto alitakiwa kucheza ndani kusaidia kiungo (inapohitajika) eneo la kati na pia kucheza kama winga kumiliki mpira kungesaidia kupunguza mashambulizi kila muda pia kuongeza ufanisi kwenye eneo la kiungo haswaa kwenye kupiga ‘key passes’ ndio maana pamoja na Simba kuwa pungufu bado ndio waliiongoza kwa kumiliki mpira kutokana na kuwa na watu kama hawa kwenye kiungo.
UCHEZAJI NA MBINU ZA MABADILIKO (STYLE OF PLAY AND TACTICAL SUBSTITUTION)
YANGA:
Yanga walionekana kuanza mpira kwa kujilinda zaidi wakijaribu kupooza mpira wakitegemea mipira mirefu na counter attacks mfano (goli la Tambwe) walitumia zaidi upande waliouzoea (upande wa kulia) alipokuwa akicheza Juma Mahadhi na Juma Abdul, Mbuyu Twite alionekana kucheza chini sana kuzuia na kuziba space kila wachezaji wa Simba (washambuliaji) walipotaka kufanya stretching, Kamusoko akishuka chini kuchukua mipira kusambaza na hii. Ndio maana Mbuyu Twite alicheza chini kuzuia plan ya washambuliaji wa Simba wasifanye kazi ndio maana Mavugo alikamatwa.
Kipindi cha pili yanga ilionekana kuzidiwa eneo la kiungo pamoja na Simba kuwa pungufu hii ni kwasababu eneo la katikati ‘transitional phase’ kuwa na wachezaji sawa yaani four vs four, wachezaji wa SIMBA wa kati ni wabunifu sana hivyo kuwafanya SIMBA waka-win midfield battle. Kosa alilolifanya mwalimu ni kumotoa Kaseke na kumuingiza Niyonzima alipaswa kumtoa mshambuliaji mmoja nakumuingiza kiungo ili kufanya idadi ya viungo kuwa 5 kwa 4 ndio maana hata Niyonzima hakuonekana.
Mfano mabadiliko aliyoyafanya Ranieri kwenye mechi dhidi ya Man United kumtoa Vardy kumuingiza kiungo Andy King kukawafanya Leicester City kuwamiliki Man United kwa sababu tayari idadi ya viungo ilikuwa 5 kwa 4 kabla then Kaseke angetoka na kuingia Msuva na kuwafanya Yanga wawe na spidi kwenye flanks lakini mwisho yote ni maamuzi ya kocha.
Badiliko la Kelvin Yondani kwa Vincent Andrew lilikuwa sahihi tayari Kelvin alikuwa na kaadi ya njano na aina ya mechi ilibidi aende nje asijepata kadi nyekundu na kuwagharimu Yanga. YANGA walionekana kucheza foul kuridhika kwani baada ya goli YANGA hawakufanya shambulizi la maana.
SIMBA:
Simba walianza mechi kwa kuwashambulia Yanga kwa kasi makini mbele walikosa mipango. Mwalimu Joseph Omog alianza na viungo wa kati watatu ili kuhakikisha ubunifu na umliki wa mpira kwa Simba uwe kipaombele yaani kiungo mkabaji mmoja (Mkude), Muzamiru na Mwinyi Kazimoto aliyekuwa anacheza kama winga wa kushoto, huku Kichuya akikamilisha idadi ya viungo akicheza kama ‘inverted winger’ pengine huyu ndiye atakuwa inverted winga bora kwa sasa uwezo wake ana kila sifa za kuwa inverted winger uwezo wake wa kupiga pasi, (mfano goli la Ajib lililokataliwa), kufunga, kupiga mashuti, alitumika kulia, sehemu ambayo YANGA ni wadhaifu ili kumtoa Haji Mwinyi kwenye nafasi yake ili aingie ndani kuacha wing na half space wazi ilinapige pasi kwa mshambuliaji (mfano goli la Ajib lililokataliwa) au kupiga pasi kwenye wing ili beki wa kulia (Bokungu) apige krosi.
Goli la Yanga ilikuwa ni uzembe wa ukabaji kutoka kwa Ajib ,alimuacha Mbuyu Twite akidribble mpira hadi kujiandaa na kupiga pasi, ambapo Ajib alikuwa anatembea na alitakiwa kukimbia, Kosa likaja kwa Lufunga akifanya ukabaji mbovu ‘poor marking’,kama beki unatakiwa uangalie mpira na position ya striker, alifanya kosa, Mwanjale nae alibaki akitazama tu, ilikuwa ni poor defence.
Baada ya kadi nyekundu ilibidi Kazimoto acheze No.8 Muzamiru No.6 Ajib acheze kushoto kama inverted wing huku Mavugo akicheza kama striker hivyo mfumo ukawa (4-4-1). Kipindi cha pili kutokana na kuwa na mshambuliaji mmoja mbele, ilihitaji typical striker na physic pia huyu ni Blagnon hivyo mabadiliko ya Mavugo yalikuwa sahihi ili kuwasumbua mabeki wa kati wa YANGA na kuwafanya wamfikirie yeye tu.
Blagnon alifanya hivyo kama ilivyotakiwa. Novert Lufunga tayari alionekana hayupo makini mechi ilimzidi uwezo alicheza rafu nyingi sana, Juko Murshid alikuwa mbadala sahihi, hii ilimfanya Method Mwanjale kuanzisha Mashambulizi na kuboost mashambulizi, alitengeneza uelewano mzuri na Murshid kiasi cha kuwazuia washambuliaji wa Yanga kipindi cha pili.
Kutolewa kwa Ibrahim Ajib ilikuwa sahihi kwa sababu upande alipokuwa anacheza ndipo upande ambapo YANGA ni imara sana,ilibidi wacheze kulia kwa Kichuya (kushoto kwa YANGA) ambapo Yanga ni wadhaifu ilibidi aongeze ufanisi kwenye kiungo na kuua winga moha na kutumia winga mmoja kumtumia Kichuya kama inverted winger ili kumtoa Haji mwinyi kwenye position Bokungu aweze kupiga krosi ili Blagnon (mfano kona ya goli ilitokana na krosi ya Bokungu na haji Mwinyi hakuwa kwenye position).
MWISHO:
Makosa ya kinidhamu, kimaamuzi, kiufundi, yawe ni funzo kwa walimu, wachezaji, waamuzi na TFF kwenye mechi hii.
Tags
MICHEZO KITAIFA