Idadi ya vifo kufuatia kimbunga Matthew nchini Haiti inakaribia watu 300, kwa mujibu wa serikali.
Katika Mji wa Jeremie asilimia 80 ya majengo yameporomoka.
Hadhi
ya Kimbunga Matthew kwa mara nyingine imepandishwa hadi ngazi ya nne,
hatua ambayo ndiyo ya pili kwa ukubwa katika mgawanyo wa aina mbali
mbali za Kimbunga, huku kikielekea katika jimbo la Florida nchini
Marekani.
Maafisa wa serikali ya Haiti wametoa takwimu mpya kuhusiana na maafa yaliyosababisha na kimbunga hicho.
Siku ya alhamisi, serikali ya nchi hiyo ilisema watu mia moja tayari walikuwa wamepoteza maisha yao. |