Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas (mwenye suti) akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum cha
360 kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha CLOUD wakati wa ziara
yake ya kutembelea vyombo vya habari Jijini Dar es Salaam na kuelezea
maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria ya huduma ya Habari.
Wengine ni Watangazaji wa Kituo hicho, Babbie Kabae (kushoto) na Hassan
Ngoma.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akibadilishana mawazo na Watangazaji wa kipindi cha Michezo cha
kituo cha Redio cha CLOUDS FM cha Jijini Dar Es Salaam, kutoka kutosho
Shafii Dauda (kulia) na Mbwiga mbwiguko (katikati) wakati wa ziara yake
ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam.
Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui
mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas (mwenye suti) akiwa katika picha ya pamoja na Wahariri na
Waandishi wa Habari wa kituo cha habari cha Redio na Televisheni cha
CLOUD wakati wa ziara yake ya kutembelea vyombo vya habari leo Jijini
Dar es Salaam. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia
maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya
habari.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akipokelewa na Meneja vipindi wa kituo cha redio cha Times FM cha
Jijini Dar es Salaam, Amani Misana wakati wa ziara yake ya kutembelea
vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es Salaam. Katika ziara hiyo
Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo
katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha
Redio cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam, Rehure Nyaulawa akifafanua
jambo kwa Mkurugenzi wa Habari, Hassan Abbas kuhusu utendaji kazi wa
gari la urushaji matangazo ya nje. Katika ziara hiyo Msemaji huyo wa
Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali yaliyopo katika muswada wa
sheria ya huduma ya habari.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akizungumza katika ya kipindi mahojiano maalum ya kipindi cha
Hatua Tatu kinachorushwa na kituo cha Redio cha Times FM cha Jjijini Dar
es Salaam kuelezea maudhui mbalimbali yaliyopo katikamuswada ya sheria
ya huduma ya Habari. Anayefuatilia mahojiano hayo ni mahojiano hayo ni
mtangazaji wa kituo hicho Stanslaus Lambat.
Mkurugenzi wa Habari, Hassan
Abbas akiwa katika picha ya pamoja na Bodi ya Uhariri ya Kituo cha Redio
cha Times FM cha Jijini Dar es Salaam wakati wa ziara yake ya
kutembelea vyombo mbalimbali vya habari Jijini Dar es Salaam. Katika
ziara hiyo Msemaji huyo wa Serikali alizungumzia maudhui mbalimbali
yaliyopo katika muswada wa sheria ya huduma ya habari.
(PICHA NA ISMAIL NGAYONGA)
………………………………………………………………………………
Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam
SERIKALI imesema hakutokuwa na
matumizi mabaya ya mamlaka anayopewa Waziri anayesimamia tasnia ya
habari katika muswada wa sheria ya huduma ya habari isipokuwa kwa
masuala yatakayohatarisha usalama wa Taifa.
Imesema Serikali haiwazuii
waandishi wa habari kukosoa sera, matamko na ahadi mbalimbali
zinazotolewa na Viongozi wa kitaifa pindi wanaposhindwa kutekeleza
maagizo wanayoyatoa kwa wananchi.
Akizungumza katika mwendelezo wa
ziara yake ya kutembelea vyombo mbalimbali vya habari leo Jijini Dar es
Salaam, Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Hassan Abbas alisema
muswada huo unatoa fursa kwa chombo cha habari kupeleka malalamiko yake
mahakamani pindi inapotokea kutokubaliana na hatua itakayoweza kuchuliwa
na Waziri mwenye dhamana ya habari.
Kwa mujibu wa Abbasi alisema
yapo masuala kadhaa yanayopaswa kuchuliwa hatua za haraka za maamuzi
ikiwemo suala la uchochezi, uasi wa kikundi fulani cha watu kinachotaka
kuigombanisha Serikali na wananchi.
Aliongeza kuwa hata katika
mikataba ya kimataifa ikiwemo kifungu cha 19 mkataba wa geneva wa mwaka
1966 umeeleza kuhusu haki ya kupata habari na taarifa ingawa upo ukomo
katika masuala kadhaa ikiwemo suala la usalama wa taifa.
“Uchochezi ni kuhatarisha amani
ya nchi, lakini mwandishi akiikosoa Serikali haitokuwa uchochezi bali
kwa atakayeleta habari za uchochezi kwa maana ya uasi atatakiwa
kuwajibishwa” alifafanua Mkurugenzi Abbas.
Aidha alisema kuwa muswada huo
umekusudia kuanzishwa kwa Baraza la Maadili litakalokuwa na wajumbe
saba, ambapo wanne kati yao ni kutoka katika tasnia ya habari ikiwemo
mwenyekiti wa Baraza na watakuwa na mamlaka ya kusimamia maslahi na
usalama wa waandishi.
Akifafanua zaidi alisema kuwa
lengo la Serikali ni kuhakikisha kuwa mchakato wa kupata Sheria ya
huduma ya habari unafika mwisho ambapo mchakato wake umechukua miaka 20
mpaka sasa.
Alisema kuwa lengo la Serikali ni
kuhakikisha kuwa muswada huo unapitishwa na Bunge ili uweze kuwa sheria
kamili na hatimaye kuifanya tansia ya habari kuwa taaluma yenye
kuheshimika zaidi.
Pia alisema kuwa muswada huo
utasaidia sekta ya habari kuwa muhimili wenye nguvu na taaluma
iliyokamilika yenye haki zake kama upatikaji wa bima za afya kwa
waandishi wa habari.
Abbasi alisema iwapo sheria hiyo
itapitishwa itatumika upande wa Tanzania Bara pekee na si Zanzibar, kwa
kuwa suala la habari halipo katika mambo ya Muungano, ingawa sekta hizo
zinashirikiana kwa namna moja au nyingine.
Tags
HABARI KITAIFA