Usiku wa Jumamosi ulikuwa ni maalum kwa mshambuliaji Liverpool Daniel Sturridge.
Sturridge alianza kwenye kikosi cha kwanza cha England kilichocheza dhidi ya Malta ikiwa ni mchezo wa kwanza kwa Gareth Southgate akiwa kama kocha wa timu ya taifa.
Star huyo wa Liverpool amekuwa akiandamwa na majeruhi ya mara kwa mara kwenye misimu ya hivi karibuni, dakika ya 29 alifunga bao la kwanza kwenye mchezo huo wa kuwania kufuzu kucheza Kombe la Dunia mwaka 2018.
Dele Alli alifunga bao la pili sekunde kadhaa kabla ya mapumziko dhidi ya Malta ambao wanashika nafasi ya 176 kwenye orodha ya FIFA.
Sturridge anayepambana kuwania nafasi kwenye kikosi cha Jurgen Klopp dhidi ya mshambuliaji wa Brazil Roberto Firmino, alifunga goli hilo akiunganisha krosi ya mchezaji mwenzake wa Liverpool Jordan Henderson
Goli la Daniel Sturridge dhidi ya Malta ni bao lake la kwanza kwa England kwenye uwanja wa Wembley tangu mwaka 2014.
Amemaliza ukame wa kucheza mechi 6 bila kufunga goli kwenye klabu na taifa, ambacho kilikuwa kipindi kirefu zaidi bila kufunga tangu May hadi Septembe 2012.
Lilikuwa ni goli la 100 kwenye maisha yake professional soka.
Sturridge amefunga mara 55 akiwa na Liverpool, magoli 24 akiwa Chelsea, 8 akiwa na Bolton,7 kwenye timu ya taifa na magoli 6 akiwa na Man City.
England iliingia kwenye mchezo dhidi ya Malta imeshinda mechi zake 13 za kufuzu Kombe la Dunia huku Simba hao watatu wakiwa hawajapoteza mchezo kwenye mechi zao 30 za mwisho za kuwania kufuzu (wameshinda 23, na kutoka sare 7).
Tags
MICHEZO KIMATAIFA