BANDA MEDIA BLOG

Hii ndiyo siri ya Mama Yanga ‘kuzima’ uwanjani Yanga ikifungwa

Shabiki wa klabu ya Yanga anayefahamika kwa jina maarufu la Mama Yanga, amefichua siri ambayo huenda wengi huwa wanajiuliza bila kupata majibu sahihi na kubaki na maswali mengi vichwani mwao.
Mama Yanga amesema kitu ambacho watu wengi hawakijui kuhusu yeye kuzimia pindi Yanga inapofungwa huwa ni mshtuko au mshangao ambao hupelekea kuanguka na kupoteza fahamu.
Mwanamama huyo maarufu zaidi kwa upande wa mashabiki wa wanawake alitoboa siri hiyo alipokuwa anazungumza na kipindi cha Sports Extra kilichokuwa kikiruka live kutoka Sabasaba Classic Bar maeneo ya Sabasaba-Mbagala ambapo naye pia alikuwa miongoni mwa wadau wa soka waliokuwepo kutoa maoni yao juu ya masuala mbalimbali ya soka.

“Huwa napata mshtuko mara nyingi pale napo shuhudia timu yangu inafungwa goli ambalo linatufanya kuwa nyuma. Hali hiyo huwa inanifanya nipate mshtuko uliopitiliza na hatimaye kupoteza fahamu,”  alisema mama huyo mwenye mwili ‘nyumba’ ambaye mara kadhaa ameshuhudiwa akisaidiwa na watu wa msalaba mwekundu baada ya kupoteza fahamu.
Moja ya picha inashoonesha Mama Yanga akisaidiwa kupandishwa kwenye gari la kubebea wagonjwa mara baada ya kupoteza fahamu baada ya timu yake kuruhusu bao dhidi ya Tanzania Prisons msimu uliopita kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya
Moja ya picha inashoonesha Mama Yanga akisaidiwa kupandishwa kwenye gari la kubebea wagonjwa mara baada ya kupoteza fahamu baada ya timu yake kuruhusu bao dhidi ya Tanzania Prisons msimu uliopita kwenye uwanja wa Sokoine, Mbeya
“Lakini nawashukuru wachezaji wetu, wanaponiona nimebebwa huwa wanapamaba kuhakikisha wanasawazisha. Hiyo imeshatokea msimu uliopita Tanga tulipocheza na Coastal Union na Mbeya tulipocheza na Prisons, baadae nikipata fahamu naambiwa tumeshinda au tulisawazisha.”
Mama Yanga amesema mapenzi yake na timu hiyo ya mtaa wa Twiga na Jangwani ni sawa na baba yake mzazi
“Jinsi ninavyoipenda Yanga siwezi hata kueleza yani, ndio maana kila inaposafiri lazima niongozane nayo. Mapenzi yangu kwa Yanga ni sawa na ninavyompenda baba yangu wa kunizaa, Yanga ni kila kitu kwangu.”

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG