BANDA MEDIA BLOG

Sare ya Arsenal vs Spurs yaweka rekodi mpya EPL

3Washika Bunduki wa jiji la London Arsenal leo wamekaliwa kooni na mahasimu wao Tottenham Hotspur baada ya kulazimishwa sare ya bao 1-1, mchezo uliochezwa katika Uwanja wa Emirates maskani kwa Arsenal.

Arsenal walipata bao la uongozi kipindi cha kwanza baada ya beki wa Spurs Kevin Wimmer kujifunga mwenyewe kufuatia mpira mzuri wa adhabu ndogo uliopigwa na Mesut Ozil.
Kipindi cha pili Spurs walikuja vizuri na kufanikiwa kusawazisha bao kwa mkwaju wa penati uliopigwa na Harry Kane baada ya Laurent Koscielny kumfanyia madhambi Mussa Dembele.
Dondoo muhimu
  • Arsenal vs Spurs ndiyo mchezo pekee wa Premier League uliozalisha magoli mengi zaidi (139)
  • Mauricio Pochettino ni meneja wa kwanza kabisa kuwahi kutokea ambaye hajapoteza katika michezo mitano dhidi ya Arsenal.
  • Harry Kane kwa sasa amefikia rekodi ya Gareth Bale kuwa mchezaji wa Spurs aliyefunga magoli mengi zaidi (magoli 5).
  • Tottenham hawajafungwa kwenye michezo 11 tangu msimu wa ligi uanze, ikiwa ni mara ya kwanza tangu msimu wa 1960-61.

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG