
Dk John Mboya Mkurugenzi Msaidizi Uwekezaji Wizara ya Viwanda na Biashara akifungua semina ya Mlipa Kodi iliyotolewa na Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA kwa wafanyabiashara wa China waishio na kufanya biashara nchini Tanzania Katika sekta ya Ujenzi na biashara zingine iliyofanyika kwenye ukumbi wa BOT jijini Dar es salaam leo, Kutoka kulia ni Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma za Kodi na Elimu kwa Mlipa Kodi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na katikati ni Bw. Yang Tong Mwambata wa Siasa Katika Ubalozi wa China.

Bw. Yang Tong Mwambata wa Siasa Katika Ubalozi wa China akitoa neno kutoka serikali ya China kwa wafanya biashara wa China wanaofanya biashara nchini Tanzania kuhusu umuhimu wa kulipa kodi ,kushoto ni Dk John Mboya Mkurugenzi Msaidizi Uwekezaji Wizara ya Viwanda na Biashara na kulia ni Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma za Kodi na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA)

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji (TIC)Bw. Cliford Tandali akiwahimiza wafanyabiashara hao kuwekeza nchini lakini pia kulipa kodi wakati wa semina hiyo.

Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma za Kodi na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) akizungumza na wafanyabiashara hao wakati wa semina hiyo.

Bw. Yang Tong Mwambata wa Siasa Katika Ubalozi wa China,Kaimu Mkurugenzi wa Kituo Cha Uwekezaji (TIC)Bw. Cliford Tandali na Dk John Mboya Mkurugenzi Msaidizi Uwekezaji Wizara ya Viwanda na Biashara wakiwa katika picha ya pamoja na washiriki wengine katika semina hiyo.

Richard Kayombo Mkurugenzi wa Huduma za Kodi na Elimu kwa Mlipa Kodi (TRA) akihijiwa na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina hiyo.

Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Uwekezaji TIC Bw. Cliford Tandali akihijiwa na waandishi wa habari mara baada ya ufunguzi wa semina hiyo.

Baadhi ya maofisa na wakuu wa vitengo kutoka Mamlaka ya Mapato TRA wakiwa katika semina hiyo tayari kwa kutoa semina kwa wafanyabiashara hao.

Picha mbalimbali zikionyesha baadhi ya wafanyabiashara wa kichina wakiwa katika semina hiyo

Tags
HABARI KITAIFA