BANDA MEDIA BLOG

ILI KUNUSURU AFYA ZA WANADODOMA, DUWASA YAWAONDOA WAKULIMA KWENYE MZUNGUKO WA MABWAWA UA MAJITAKA

Tingatinga la DUWASA likifyeka miwa, mahindi na bustani za mbogambaga zilizolimwa kandokando ya mabwawa ya maji Taka yaliyopo swaswa Manispaa ya Dodoma


Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini Christina Mndeme akionyesha moja ya miwa iliyokuwa inalimwa kandokando ya Bwawa la maji Taka swaswa, Miwa hiyo pamoja na mazao mengine vimefyekwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira [DUWASA] ili kuwanusuru watatnzania kula vitu vichafu ambavyo ni hatari kwa afya zao [PICHA NA JOHN BANDA]


Askari wa kuzuia Ghasia wakiimalisha ulinzi katika eneo hilo

Wakulima wakiendelea kuvuna nyanya zilizokuwa zikimwagiliwa na maji yaliyotolewa kwenye Bwawa la maji Taka katika eneo la swaswa Dodoma


wakaulima wakipita katika shamba lililofyekwa miwa na DUWASA ili kupisha hifadhi ya maji taka

kazi ikiendelea

Tingatinga likiendelea na kazi chini ya ulinzi mkali wa polisi



Na John Banda, Dodoma
MAMLAKA ya maji safi na usafi wa mazingira mjini Dodoma  [DUWASA] Imefanya Oparationi ya kuwaondoa wakulima 88 waliokuwa wakilima Bustani za mbogamboga, mahindi na miwa, kandokando ya mabwawa ya maji taka yaliyopo Swaswa mjini hapa
Katika Oprationi hiyo iliyokuwa na ulinzi mkali wa polisi chini ya Mkuu wa Wilaya ya Dodoma mjini Christina Mdeme magreda na vifaa vingine kama mapanga, makwanja na majembe yaliyokuwa yakitumiwa na vijana maalumu waliopelekwa rasmi katika zoezi hilo na DUWASA
Akiongea na waandishi wa habari  wakati zoezi hilo likiendelea Mkuu huyo wa wilaya alisema utekelezaji huo unafanywa kutokana na agizo la Naibu waziri  Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira Luhaga Mpina aliyefika katika eneo hilo hivi karibu wakati wa ziara maalum na kuagizo wakulima hao waondolewe  ili kunusuru afya za wananchi
Mndeme alisema kitendo cha kulima mazao ya chakula kama mbogamboga, miwa, mahindi na hata migomba kwa kumwagilia maji machafu kiasi kile ni ukiukwaji mkubwa wa sheria ya Afya na mazingira hali inoweza kusababisha afya za binadamu kuwa hatarini
“pamoja na kuweka doria za mara kwa mara ikiwemo kupanda miti na ukoka katika maeneo yote yanayozunguka bwawa hili pia nitoe tahadhari kuwa tutamchukulia hatua kali za kisheria mtu yoyote ambaye atakamatwa akipampu maji hayo machafu kwa ajili ya kumwagilia bustani”, alisema
Kwa upande wake Afsa Afya wa manispaa Alecky Barankena alisema mazao hayo ambayo yamekuwa yakilimwa katika maeneo hayo husababisha athari za magonjwa ya tumbo kama taiphod, Kipindupindi, minyoo, figo na hata salatani hivyo ili kuzuia hali hiyo ni kuacha kutumia maji hayo kumwagilia mazao yao
Alisema mwaka jana katika maeneo yote yanayozunguka eneo hilo za ipagala, kwa mwatano, ilazo na swaswa yenyewe mwaka jana kulikuwa na mlipuko mkubwa wa kipindupindu na walio wengi walikuwa wakilima kandokando ya bwawa hilo
Nae Ofsa mawasiliano wa mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Sebastian Wariaoba alisema Oparation hiyo ni ya kuwaondoa wakulima wote waliokuwa katika hifadhi ya mabwawa hayo ambapo hawakutakiwa kuingia ndani ya mita 100 toka mabwawa yalipo
Mwenyekiti wa wakulima hao Elia Yohana alisema wao hawapingani na sheria japo wanajua kuwa wataathirika kwa kiasi kikubwa kutokana na wengi wao wanamikopo lakini pia familia zitakosa kujiendesha kwa kuwa hata hivyo wamekuwa wakifanya kilimo hicho kwa kipindi cha miaka 36 wao wakiwa 88

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG