Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
amemuagiza Waziri na Katibu Mkuu katika Ofisi ya Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI) kusitisha mara moja utekelezaji wa zoezi la
kuwaondoa wafanyabiashara wadogo maarufu kwa jina la Machinga katika
Jiji la Mwanza pamoja na mikoa mingine mpaka hapo mamlaka husika
zitakapokamilisha maandalizi ya maeneo watakapohamishiwa na kwa
kuwashirikisha wamachinga wenyewe.
Rais Magufuli akiwa na Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan ametoa
agizo hilo tarehe 06 Desemba, 2016 Ikulu Jijini Dar es Salaam huku
akionya kuwa kiongozi yeyote ambaye hayupo tayari kutekeleza agizo hilo
aachie ngazi.
