| Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na ufundi Prof, Joyce Ndalichako akisisitiza jambo wakati alipokuwa akifngua mkutano wa umoja wa walimu wakuu wa shule za sekondari uliofnyika mjini Dodoma |
| Rais wa umoja wa walimu wakuu wa shule za sekondari akizungumza katika mkutano huo |
| Mkurugenzi wa Global Education Link akipokea tuzo ya umahili wa kuchangia Elimu Nchini toka kwa Waziri wa Elimu, sayansi, Teknolojia na ufundi Prof, Joyce Ndalichako [PICHA NA JOHN BANDA] |
| Walimu wakuu sekondari wakiwa katika ukumbi wa nyerere Dodoma wakati wa mkutano huo |
Na John Banda, Dodoma
WAZIRI wa
Elimu,Sayansi,Teknolojia na Ufundi,Prof.Joyce Ndalichako, amesema Walimu wakuu
nchini wanatakiwa amewataka kusimamia
ubora wa elimu kutokana na wao kukaa karibu na wanafunzi.
Akizungumza jana Mjini hapa wakati akifungua Mkutano Mkuu
wa Mwaka wa Wakuu wa Shule za Sekondari Tanzania (TAHOSSA) Prof.Ndalichako alisema
Walimu Wakuu wanawajibu wa kusimamia ubora wa elimu nchini.
Alisema wao
ndio wanakaa na wanafunzi hivyo wanawajibu wa kuwa wasimamizi na wakaguzi wa kwanza
ili kuiboresha elimu ya Tanzania.
Pia alisema
elimu ya Sekondari ni kiungo muhimu katika kuendeleza elimu nchini kwani hapo
ndipo wanapotoka wanafunzi wataoenda katika vyuo vikuu na vyuo vya kati.
‘’Serikali
itaendelea kuimarisha elimu ya sekondari pia tunaomkakati wa kuimarisha
ufundishaji wa masomo ya Sayansi’’alisema Profesa Ndalichako.
Pia alisema
kwa sasa utaratibu watakaotumia kuajiri
walimu wa Sayansi kwa sasa umebadilika kwani wale wote waliohitimu Ualimu wa
Sayansi na Hisabati wanatakiwa watume vyeti vyao kabla ya kupangiwa kituo cha
kazi.
‘’Kwenye
Arts tuna walimu wa ziada hao tutajaribu kuwapanga kutokana na shule kwani
wengi walikuwa wamepangwa shule moja hivyo tutaangalia utaratibu wa kuwapanga
kulingana na mahitaji’’alisema
Pia
aliwataka Walimu Wakuu hao kuhakikisha wanasimamia ubora wa elimu nchini kwani
wao ndio wanaowapika wanafunzi kabla ya kwenda vyuoni.
Vilevile
aliwataka Wakuu hao kupeleka takwimu sahihi za wanafunzi waliopo katika shule
zao ili kuisaidia serikali katika kupanga bajeti ili iweze kutoa fedha sahihi.
‘’Hapa kuna
kimbembe wakati mwingine huwa najifanyisha nimepoteza takwimu ya shule fulani
nikitumiwa inakuwa tofauti na ile ya mwanzo niwaombe walimu mkalisimamie hili
ili iwe rahisi kwetu kupanga bajeti yenye tija’’alisema
Aidha Prof.
Ndalichako alisema kutokana na maabara nyingi kukamilkia serikali itatoa vifaa
vya maabara kuanzia Januari mwaka huu kwani kwa sasa ndio vimeagizwa.
Kuhusina na
mimba wanaopewa wanafunzi,Profesa Ndalichako alisema ni changamoto kubwa kwao
na wameunda Kamati ya kushughulikia suala hilo ambayo itampa majibu katika siku
za hivi karibuni.
Aidha Waziri
huyo alisema Makatibu Tawala na Wakurugunzi kuwalinda walimu wanaofuata
kanuni,taratibu na sheria katika utendaji kazi wao likiwemo suala la wanasiasa
kuingilia masuala ya elimu.
‘’Wanasiasa
wamekuwa wakiingilia suala la elimu niwaombe Wakurugenzi na Makatibu Tawala
kulishughulikia suala hilo kwa kuwalinda walimu wakuu ambao wanafuata
kanuni,sheria na taratibu’’alisema
Pia
aliwataka Walimu wakuu kuwa na mahusiano mazuri na jamii inayowazunguka pamoja
na kufanya usafi katika shule zao.
‘’Unafika
shule mapaka unajuliza kuna watu wanaishi hapa niwaombe mjitahidi katika suala
la usafi ikiwezekana muwe na siku maalum ya kufanya usafi’’alisema
Akisoma
risala Rais wa Tahossa,Bonus Nyimbo
aliiomba serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa wanafunzi mashuleni kwani
imekuwa ikichangia kushusha ufaulu wa baadhi ya wanafunzi.
Nyimbo
ambaye ni mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mwenge ya Mkoani Singida aliiomba
serikali iajiri walinzi,watumishi na madereva ili waweze kufanya kazi kwa
ufasaha.
Alisema
changamoto nyingine wanayokabiliwa nayo ni baadhi ya wanachama kutoelewa vizuri
katiba pamoja na kutokulipa ada kwa wakati.
‘’Ili kuboresha
elimu tunaiomba serikali itoe waraka wa kupiga marufuku matumizi ya simu kwa
wanafunzi kwani simu nyingi tunazozikamata tunakuta mule hakuna
taaluma’’alisema
Kwa upande
wake Mkurugenzi wa Global Education Link,AbdulMalik Molel ambaye kampuni yake ilipewa tuzo ya heshima katika
kuendeleza elimu nchini,alisema ni jukumu la kila mmoja kutimiza wajibu wake
ili kuiendeleza elimu ya Tanzania.
‘’Kila mmoja
anapaswa kutimiza wajibu,Wazazi,Walezi,Walimu Waambieni wanafunzi wasiwe na
‘Expection’ kwani wakienda vyuo vikuu wanakuwa wasumbufu’’alisema
Tags
ELIMU