
Na.Alex Mathias.
Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara Yanga SC imeifanyia maafa timu ya Jamhuri ya Pemba jumla ya magoli 6-0 mchezo wa Michuano ya Kombe la Mapinduzi kwenye uwanja wa Amani mjini Zanzibar.
Yanga walipata magoli yote manne kipindi cha pili kupitia kwa washambuliji wake wanaotisha katika Ligi ya Tanzania bara Simon Msuva na Donaldo Ngoma.
Msuva alifunga mawili dakika ya 19 akiunganisha mpira wa kona ya Haruna Niyonzima na 40 akipokea pasi ndefu toka kwa Thabani Kamusoko na Msuva aliweza kumvisha kanzu golikipa.
Donaldo Ngoma naye alifunga mawili dakika ya 23 baada ya kupokea pasi ya Haji Mwinyi aliyekuwa kwenye fomu ya mchezo na 36 baada ya mlinda mlango kupangua shuti la msuva na kumkuta mfungaji akiwa kwenye nafasi nzuri hadi mapumziko Yanga walikuwa mbele kwa magoli manne.
Kipindi cha pili kilianza kwa Jamhuri kuingia kwa kasi huku wakitaka kupata angalau hata bao moja la kufutia machozi na dakika ya 59 Thabani Kamusoko alipingilia msumari wa tano akipokea pasi ya mtoto wa Kizanzibar Emanuel Martin.
Akitokea benchi kiungo mshambuliaji Juma Mahadhi alifunga goli la 6 dakika ya 85 akipenga bonge la goli kwa shuti la mbwa Mwitu na kumuacha golikipa hana la kufanya.
Mpaka dakika 90 zinamalizika Yanga wameibuka na ushindi wa magoli 5-0 na kuongoza kundi B wakiwa na pointi zao tatu wakiwa sawa na Azam FC ila Yanga wakiwa wana magoli mengi ya kushinda.
Michuano hiyo itaendelea kesho ikiwa ya Kundi A michezo miwili kupigwa mchezo wa mapema utakuwa saa 1:00 kati ya URA na Taifa Jang’ombe boys na majira ya usiku saa 2:15 Simba atavaana na KVZ mchezo unaotabiriwa kuwa mkali.
Tags
MICHEZO KITAIFA