Kama kichwa cha Habari kinavyojielezea mimi ni binti mrembo tu Nina kaxi
yangu nzuri Namshukuru Mungu, nimepita kwenye mahusiano kadhaa
changamoto hazikosekani Nimekutana na wenye uwezo wanaoweza kanipa
Nitakacho na wenye uwezo wa kawaida tu.
Nilichojifunza ni kwamba Unaweza kuwa kwenye mahusiano na mtu Anaejiweza
akakupa kila utakacho ila hana muda na wewe hamna out wala muda wa
kukaa mkayajenga hata mazungumzo ya kawaida maana mimi ni mpambanaji
Mkikutana ni show basi siku zinaenda mwaka umekatika hamna la maana na
sio kwamba anamahusiano mengine Hapana ingawa Mwanaume huwezi msemea ila
ni mtu ambaye uko nae huru ila yuko busy muda wote hawezi kujenga muda
kwa ajili yako ila muda wa kufanya mengine kama kwenda Bar, karaoke nk
anao
Pili Mwanaume Ambae hawezi kukuhudumia kwa chochote mnapata muda wa
kuzungumza kushauriana kupanga Mambo ya maendeleo ingawa hamuwezi kwenda
out nk kutokana na kipato ila mapenzi mnayafurahia hata kwa kukaa ndani
tu coz mimi sio mtokaji na haijawahi kunipa chochote wala sijawahi
kumuomba coz namjua Hali yake
Ingawa ana wasiwasi na mimi kutokana na uwezo wake na urembo wangu ila
mimi sina tatizo coz najimudu kwa kila kitu. sasa huyo mwenye uwezo
miezi4 hatuko vizuri na naona nimeshindwa mimi kwa moyo mweupe coz
sijawahi kuenjoy nae hata siku moja nataka kumpokea huyu wa Hali ya
kawaida kwa moyo mmoja tujenge familia maana kule naona utumwa naombeni
Ushauri ndugu zangu
By Vantz
Tags
MAHUSIANO
