Iliwashangaza wengi baada ya Vanessa Mdee naye kutajwa kwenye orodha ya
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ya mastaa wanaohusishwa na
biashara ya madawa ya kulevya. Ni shutuma nzito, na hata kabla
uthibitisho rasmi haujatoka, madhara ya kutajwa majina yao yameanza
kuonekana katika maisha yao
Wito huo umemkutia Vee Money akiwa nchini Afrika Kusini anakoshoot
tamthilia ya MTV Shuga, na bila shaka atalazimika kukatisha kwa muda na
kurudi Tanzania kwenda kituo cha polisi central, anakotakiwa Jumatatu ya
kesho.
Pamoja na hivyo, Vee ameonesha kuvuta pumzi ndefu na kuacha maisha
yaendelee kama yalivyo. Kupitia Instagram, Vee amepost picha hizo juu na
katika ile aliyokaa ameandika: The show must go on … bomb ass dress
from @asos #FILA.
Kwenye hiyo black and white ameandika: The night is darkest before the dawn. #Breakthrough #Juu #CashMadame #SheKing.”
Kwenye picha hizo amezima comments ili kuepuka maneno ya kejeli kutoka
kwa baadhi ya watu ambao tayari wamefanya hivyo kwenye picha zingine.
Vee anaungana na mastaa wengine wakubwa wakiwemo Wema Sepetu, Mr Blue,
TID na wengine kwenye orodha hiyo.
Tags
BIASHARA HARAMU
