Wasomi wengi wanapoangalia suala la akili kuna vitu wanasahau. kuwa kuna
multiple intelligence. or variety of intelligence. unaweza ukawa na
akili ya darasani au akili ya uwanjani ikiwa umchezaji wa mchezo flan.
Michael Jackson alikuwa na akili ambayo wakati mwingine watu wanaamua
kuita kipaji. ukiangalia music aliokuwa akiimba na kucheza michael
jackson utagundua kuwa alikuwa anatumia akili nyingi sana kuuandaa na
kufaham aucheze vipi. Angalia namna ambavyo majukwaa yake yalikuwa
yanaandaliwa. wakati flan mpaka kifaru kilikuwa kinaletwa jukwaani.
Angalia tamasha alilolifanya live huko munich ujeruman. wajeruman maelfu
walifurika jukwaani wengi wao hata english hawakuwa wakiijua lakini
waliimba naye, wengine walizimia kwa hisia, walilia kwa kusikiliza tu
maneno ambayo hawakuwa wakijua maana yake. lakini namna alivyokuwa
akicheza na kuonesha hisia zake kwenye maneno hayo nao pia walikuwa
wakijihisi wanaelewa na kusikia ile hali aliyokuwa akiisikia.
Hii ni kutokana na utunzi wa kiakili na uimbaji pia. utaona pia katika
tamasha hilo jinsi ambavyo aliandaa mpaka kifaru kuja jukwaani na
mazingira mbalimbali katika wimbo wake wa "What about us"
Akili si walikuwa nazo akina Aristotle,Socrates,Archimedes, Einstein
etc. tukiangalia kwa upande huu mwingine pia ni akili nyingi zilitumika
kwa yeye kuweza kuteka nyoyo za watu namna ile. kama ni mtu mwenye
kuamini ushirikina ungesema aliwaroga ndio maana alipendwa kila sehemu.
Sikiliza mashairi ya nyimbo zake. kama huna akili huwezi tunga mashairi
yale. angalia video zake. ambazo pia zilikuwa na maelekezo yake mengi
anataka video iweje. Hii yote ni akili. wadau tunapowaza suala la akili
tusiangalie upande mmoja tukasahau kila mtu ana akili zake kwa eneo
lake.
Aina yake ya uchezaji ambayo ilikuwa ni ya kimapinduzi ni uvumbuzi
alioufanya ukiangalia ile style ya moon walker au angalia ule ubunifu wa
kwenye wimbo wa smooth criminal pale inapoonekana ameweza kuishinda
gravitational force.
Anaenda mwili mzima yeye na wachezaj wake na kurudi pasipo kuanguka.
umejiuliza aulitumia mbinu gani? Huoni kama hiyo ni akili kwa lolote
alilolifanya?
Tumkumbuke kama mmoja ya watu waliokuwa na akili na wenye mchango wa
kipekee hapa duniani. Kwa kupitia music wake wengi walikuwa motivated
kuimba na kucheza na wengi waliburudishwa na kuelimishwa.
Tags
KIBURUDANI
