BANDA MEDIA BLOG

No title

MWENYEKITI YA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA YA WILAYA YA DODOMA MJINI, JABIR SHEKIMWERI AAGIZA STENDI YA DALADALA MAKOLE IANZE KUFANYA KAZI IFIKAPO NOV MOSI MWAKA HUU.

Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri akitoa maelekezo kwa viongozi wa kata ya makole kuhakikisha waliokuwa wamiliki wa nyumba zilizolipwa fidia na serikali kuzibomoa na kuondoa vitu vyao bila kupata hasara, ili kupisha ujenzi wa stend ya daladala, 
Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri akitoa maelekezo kwa y jambo kwa Diwani wa kata hiyo Omary Omary


Mweyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri akitoa maelekezo ya ukamilishwaji wa zoezi hilo ifikapo mwishoni mwa mwezi huu



Muonekano wa mabanda ya mbao na mirunda ambayo yanatakiwa kuondolewa ili kupisha utanuzi wa stendi ya daladala katika eneo la makole

              ................................................

               NA MWANDISHI WETU, DODOMA

MWENYEKITI  wa kamati ya ulinzi na Usalama Wilaya ya Dodoma mjini Jabir Shekimweri  amemuagiza Mkurugenzi wa jiji hilo Kuhakikisha Stendi na Soko lilipo D' Centre ya Makole kufunguliwa Ifikapo Nov Mosi Mwaka huu.

Aidha kuhusu kipande cha Ardhi Kilichomegwa katika sehemu ambayo awali ilitengwa kwa ajili ya kujenga paa kwa ajili ya wauza mbogamboga na Matunda na kuwaongezea kanisa la Roman Ctholic, amewataka wahusika kusema kama wamebadilisha ramani.

Akiongea katika D, Centre hiyo ambayo ilitengwa na Iliyokuwa CDA tangu mwishoni mwa miaka ya 1970  kwa ajili ya Stendi na Soko la Jamii wakati alipofanya ziara ya kushtukiza amesema Soko Hilo wahusika wafike kwa ajili ya kukagua Miundombinu iliyopo na kuhakikisha linaanza kazi mwanzoni mwa mwezi ujao.

"Niombe Afisa Biashara, Jeshi la zimamoto, LATRA, Afsa Afya Mkiwa Chini ya Afsa Tarafa  piteni kukagua na kujiridha kuhusu Miundombinu hasa ya vyoo na maji ili ifikapo muda huo Stendi I we imefunguliwa na kuanza kufanya kazi.

Aidha ameuagiza uongozi wa Kata ya Makole Kuhakikisha Nyumba zote zilizolipwa fidia tangu mwanzoni mwa mwaka huu kuondoa vitu vyao na waliovamia kujenga vibanda vya mbao kuondoaka ili kupisha eneo Hilo limwagwe kifusi na kusawazishwa pamoja na kusafishwa kwa ajili kupisha daladala..

Awali Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabiashara wa D Centre, hiyo John Banda amesema kuwa zaidi ya vibanda vya block vimejengwa katika eneo Hilo kwa Nguvu za wafanyabiashara tangu mwaka 2017 baada ya kuhamishiwa hapo wakitokea kilipokuwa kituo cha Daladala jamatini na Sarafina walikovunjiwa

Amesema anaiomba Serikali kutimiza ahidi ya kuletewa Daladala ili Soko Hilo lifunguke ambapo itachochea mendeleo ya kata ulipaji wa Kodi na kuliongezea jiji Mapato ambayo yamekuwa yakipotea zaidi ya Miaka 5 sasa

" Mhe. Mkuu wa Wilaya iwapo jiji wangeweza kutimiza Hadi hii ya Daladala na tukakubaliana jinsi ya kulipa Kodi mfano hata kwa 20,000 kwa mwezi kila kibanda maana yake jiji kwa mwaka wangekusanya zaidi ya Bil 1. kwa vibanda Vyote 500 hvyo tunaiomba serikai itusaidia maana baadhi yetu wamekata mitaji na kuishi maisha ya kubahatisha", 

Naye Diwani wa Kata hiyo ya Makole Omary Omary   amesema hao waliojenga vibanda vya mbao na milunda walivamia hivyo atamuagiza Mwenyekiti wa mtaa huo kuwatangazia ili waondoe vifaa vyao pamoja na wenye nyumba zilizolipwa fidia kuondoka kwa ajili ya kupisha Mradi huo wa Serikali uweze kutekelezwa

 

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG