BHOKE AIOMBA SERIKALI PAMOJA NA WADAU WA MAENDELEO KUWAAMINI WATU WENYE ULEMAVU NA SAPOTI YA KUTEKELEZA MIRADI YAO
NA JOHN BANDA, DODOMA
Makamo Mwenyekiti wa Jukwaa la Uwezeshaji Kiuchumi Wanawake, Bhoke Ramadhan amewaomba Wadau pamoja na Serikali kuwatupia Macho watu Wenye ulemavu kwa kuwa wepesi Kuyapokea na Kuyajibu Maandiko yao ya Maombi fund za Kuendeshea Miradi wanayoibuni.
Bhoke ambaye ana changamoto ya Ulemavu wa Viongo, Ameyasema hayo mbele ya Waandishi wa Habari, jijini Dodoma wakati wa Mafunzo ya Ujasiriamali kwa Watu Wenye Ulemavu wa aina mbalimbali.
Amesema Walemavu wana Mahitaji Mengi ya Kujikimu hivyo Inabidi Serikali pamoja na Wadau wa Maendeleo Kuwatupia Macho na kuweza kuwawezesha ili kuweza kuendesha Shughuli zao kwa urahisi
"niwaombe wadau wa maendeleo pamoja na Serikali waweze kutuamini na kutusaidia ili tuweze kuendesha Shughuli za kijamii za kuwasaidia wenzetu kupata elimu za utambuzi",amesema
Bhoke ambaye amekuwa na Utaratibu wa Kila mwaka kufanya Mafunzo ya Ujasilia Mali Bila Malipo yoyote kwa Watu wenye Ulemavu amesema inamuwiya Vigumu kwani kuna hitajika maandalizi ya vifaa vya kufundishia na hata anapojaribu kutafuta wadau wa kumuunga mkono wanakuwa wazito.
Mbunge wa Viti Maalu Mkoa wa Dodoma, Fatuma Tofik kwenye ufunguzi wa Mafunzo hayo amewataka Walemavu Kutokuwa na Woga wa Kuchukua Mikopo hasa asilimia 4 kwa vijana, 4, kwa Wanawake na 2 kwa watu wenye Ulemavu inayotolewa na Serikali ambayo kwa sasa Mfumo wake Unarekebishwa kutokana na changamoto kadhaa zilizojitokeza awali.
Amesema hata hivyo katika Ofisi ya Waziri Mkuu Kuna Fedha za Kuwawezesha Watu wenye Ulemavu kwa Njia ya Mikopo zaidi ya Bil 1. hivyo inabidi watu wa Jamii hiyo waichangamkie...