BANDA MEDIA BLOG

No title

HIKI HAPA CHANZO CHA MASIMANGO NA MANYASOSO WANAYOFANYIWA WANAUME KATIKA NDOA  ...................!!!!

Katikati,ni Mke wa Msaidizi wa Askofu, Mariamu Tabulu, Kushoto ni Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake Dayosisi ya Dodoma, Dkt. Juliana Manyerere na Mwenyekiti wa Umoja wa Akina Mama, Kanisa Kukuu la Kati Mkoani Humo Dkt, Tumain Sanga.
Mchungaji Samwel Ngajilo wa kanisa la KKKT, Dayosisi ya Dodoma akiwa katika picha ya Pamoja na wanakwaya wa kwaya mbalimbali za kanisa Kuu la mjini Kati


Mwenyekiti wa Idara ya Wanawake Dayosisi ya Dodoma, Dkt. Juliana Manyerere, akizungumza jambo na wanawake anaowaongoza mara baada ya Ibada ya Mwaka mpya wa 2024.
                                 .........................................

                     Na John Banda, Dodoma

                     BANDA MEDIA ONE.COM

IMEBAINIKA kuwa chanzo cha ndoa nyingi kuvunjika ni kutokana na watoto wengi wa Kiume kushindwa kujisimamia na kubeba majukumu yao kama wanaume katika Familia hivyo kugeuka kuwa kama mzigo.

Pia watoto wa kike wamekuwa na nguvu kubwa katika familia kutokana na Elimu mbalimbali zikiwemo za kujitambua na kujisimamia, walizopewa kwa miaka kadhaa ya hivi karibuni.

Kutokana na hali hiyo, Idara ya Wanawake ya Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Dodoma imekuja na mkakati katika mwaka huu wa 2024, wa kuhakikisha inalivalia njuga swala la mtoto wa kiume.

Akiongea na BANDA MEDIA ONE.COM, Mwenyekiti wa Idara ya wanawake ya kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Dayosisi ya Dodoma Dkt. Juliana Manyerere amesema kwa sasa hali imebadiliaka sana kwani majukumu mengi ya familia yanabebwa na mwanawake walio wengi.

 “mtoto wa kike amefanyiwa mkakati mkubwa katika jamii ili asionewe, asinyanyaswe, ajisimamie lakini pia awe na nguvu ya kiuchumi, sasa imefika wakati mtoto wa kiume aliyekuwa kaachwa kwa muda mrefu amebaki kabweteka katika familia asijue cha kufanya,

Kibinadamu inapotokea Mwanamke ananguvu ya kiuchumi analea familia, katika nyumba lazima manyanyaso na masimango yatakuwepo kwa huyo mwanaume sasa ili ndoa hiyo iweze kusimama inahitaji neema ya Mungu la sivyo ndiyo maana unaona ndoa nyingi zinavunjika mapema”, amesema

Amesema wao kama idara ya kanisa, katika mikakati waliyonayo mwaka huu wa 2024, watahakikisha wanatoa Elimu kwa wakristo wa kanisa hilo na jamii kwa ujumla kuhusu umuhimu wa kumuelimisha mtoto wa kiume naye aweze kujisimaia na kujua majukumu yake katika familia kutakakochagizwa na nguvu ya kiuchumi.


Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG