MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR HEMED SULEMAN AFUNGUA KONGAMANO LA KUADHIMISHA MIAKA 60, YA MAPINDUZI MATUKUFU YA ZANZIBAR
.........................................................................
Serikali ya awamu ya nane (8) imeimarisha Miundombinu ya
Biashara, Afya, Elimu ,Maji safi na salama, Mawasiliano na Uchukuzi ili
kuendana na dhamira ya Mpinduzi Matukufu ya mwaka 1964 ya kuwaletea wananchi
maendeleo, sambamba na kuimarishwa kwa dhana ya uchumi wa buluu ambayo ndio
ajenda ya Kitaifa.
Akifungua kongamano la kuadhimisha miaka 60 ya mapinduzi ya
Zanzibar katika Ukumbi wa Golden Tulip Uwanja wa Ndege jijini Zanzibar Mhe
Hemed amesema malengo ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar yalilenga kuondoa ukoloni
na kuimarisha uchumi na kuwaletea maendeleo wananchi
Amesema Serikali inandelea kuimarisha miundombinu mbali mbali
ambapo kwa upande wa Afya imefanikiwa kujenga hospitali kumi(10) za Wilaya na
Hospital moja(1) ya Mkoa iliyoko Lumumba pamoja na kujenga na kukarabati vituo
vya Afya vya msingi na ujenzi wa nyumba za madaktari kwa Unguja na Pemba.
Amesema kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kujenga
shule sitini na nne(64)ambapo shule 34 ni za gorofa ikiwa lengo la Serikali ni
kufikia azma ya wanafunzi kwenda shule kwa mkondo mmoja (1) kwa idadi ya
wanafuzi arobaini na tano (45) kwa kila darasa.
Aidha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar amesema Serikali
imeimarisha mazingira bora kwa wafanyabiashara wakubwa na wadogo kwa kujenga
masoko makubwa na yakisasa yakiwemo soko la Mwanakwerekwe, Jumbi na Chuini kwa
lengo la kuwawekea wafanya biashara mazingira mazuri, pamoja na kuweka
utaratibu mzuri wa kuwapatia mikopo wajasiriamali ili waweze kujiendeleza
kiuchumi.
Sambamba na hayo Hemed amesema Serikali ya Mapinduzi ya
Zanzibar itahakikisha inayafanyia kazi mapendekezo na maazimio
yatakayotolewa katika kongamano hilo ambayo yatasaidia katika kufikia maendeleo
ya nchi pamoja na kuwataka wananchi kuendelea kuwa wasikivu na watulivu kwa kuipa
ushirikiano Serikali yao inayoendelea
kutekeleza mipango mizuri ya maendeleo.
Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe Tabia
Maulid Mwita amesema malengo ya kufanyika kwa Mapinduzi Matukufu ya Mwaka 1964,
ni kuimairisha uchumi wa Wazanzibari wazawa ambao wengi wao ni wakwezi na
wakulima, kuimarisha amani na uzalendo kwa wananchi ambapo maono na falsafa zao
zinaendelea kudumu na kuenziwa kwa maslahi ya Taifa .
Aidha amesema kuwa kufanyika kwa kongamano hilo kunatoa fursa kwa
wale wote waliozaliwa baada ya mapinduzi kufahamu dhana nzima ya kufanyika kwa
Mapinduzi ili kuweza kujua umuhimu wake na namna ya kuyalinda na kuyaenzi
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Nao watoa mada katika kongamano hilo wamesema kuwa kufanyika kwa
Mapinduzi Matukufu ya mwaka 1964 yalikuwa na lengo la kumkomboa Mzanzibari na
mazila makubwa na utumwa waliofanyiwa na wakoloni kwa lengo la kujitawala na
kufanya maamuzi yao wemyewe.
Wamesema kuwa mapinduzi ndio yaliyowajenga viongozi na wananchi
kuwa wazalendo na nchi yao na kuwepo kwa Maendeleo, kuimarika kwa Amani
na Utulivu, Upondo na mshikamano mambo ambayo hadi sasa yanazidi kuimarishwa na
Serikali ya awamu ya nane (8) na kufikia ile dhamira ya waasisi wa Mapinduzi
yaliyoongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar marehemu