
Umoja wa Mataifa nchini Somalia, UNSOM umelaani vikali shambulio la makombora lililomuua afisa wa Kitengo cha Ulinzi cha Umoja wa Mataifa siku ya Alhamisi.
"Kitengo cha Ulinzi cha Umoja wa Mataifa kina jukumu
muhimu katika kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa wanaofanya
kazi katika kuunga mkono amani ya Somalia na ujenzi wa serikali," alisema
mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia, Catriona
Laing.
"Tunalaani kitendo hiki cha unyanyasaji, na mawazo
yetu yako pamoja na familia na wafanyakazi wenzetu walioathirika wakati huu
mgumu,” Laing aliongezea,
Mashambulizi kadhaa ya makombora yalitua siku ya Alhamisi
ndani ya eneo la Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Aden Adde, ambapo Uwanja wa UN
unapatikana.
Mbali na kifo cha mwanachama wa Kitengo cha Walinzi wa
Umoja wa Mataifa, mashambulizi hayo yaliharibu miundombinu.
Al-Shabaab imeripotiwa kuhusika na shambulio hilo.
Umoja wa Mataifa nchini Somalia unatoa wito kwa wale waliohusika kufikishwa mahakamani, na bado wamejitolea kusaidia watu na serikali ya Somalia katika juhudi zao za kujenga amani na utulivu nchini humo.