Isaack Mluma akiwa nje ya Ukumbi wa Jakaya Kikwete jijini Dodoma alipohudhulia Mkutano mkuu wa Vyombo vya Utangazaji uliondaliwa na TCRA
...........................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
WAKATI Mwili wa Hayati Edward (EDO) Lowasa aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali Serikalini ikiwemo ile ya Uwaziri Mkuu na baadae Kujihudhuru akiacha Alama ya Ujenzi wa Shule za Sekondari za Kata, Mwandishi wa Magazeti ya Serikali Enzi hizo aibuka na Kutaka Nguli huyo aenziwe kwa moja ya vyuo vikuu hapa Nchini kuitwa jina lake, kama ilivyo kwa kile cha Sokoine au Nelson Mandela.
Mwandishi huyo Mkongwe aliyelianzisha Gazeti la Habari Leo mwaka 2006 ambaye Kwa Sasa ni Mjumbe wa Kamati ya Maudhui ya TCRA, Isack Mluma, akiwa kwenye mkuutano mkuu wa mwaka wa Vyombo vya utangazaji jijini Dodoma, ameidokeza BANDA MEDIA ONE.COM Kuwa Lowasa ndiye aliyehakikisha wanafunzi hawazagai hovyo mitaani baada ya kumaliza masomo ya Darasa la 7 Kwa ajili upungufu wa Sekondari.
"Mimi naonelea ili kumuenzi hasa, aenziwe kwa Moja ya Vyuo Vikuu hapa Nchini Kipewe jina la Lowasa,
Nasikia hapa Dodoma kuna chuo kikuu cha TEHAMA kinajengwa Nala, hata hicho Kitwe jina la Lowasa kwani Yeye ndiye Muanzilishi wa Shule za Sekondari za kata,
Alikuwa mkeleketwa hasa wa Elimi ya Nchi hii, Ona hata alipoona wanafunzi watakapomaliza Kidato cha 6 watakwama akaanzisha ujenzi wa Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) Lowasa alikuwa Mbunifu Sana", amesema
Mwandishi huyo ambaye aliwahi kuwa Mwandishi wa CCM, Miaka ya 1991 anamzungunza Lowasa ambaye wakati huo alikuwa Msaidizi wa Katibu Wa Siasa na Uenezi Ally Amiry kuwa alikuwa akitoa ushirikiano Mkubwa hasa katika kitengo cha habari
Mluma anabainisha kuwa Lowasa alikuwa na Kasi ya Utendaji Sana kwani mwaka 2006, yeye aliitwa Kuwa Mhariri wa Gazeti la Dairy News na hapo Lowasa akamwambia Aainzishe Gazeti la Kiswahili na katika miezi 6 awe amekamilisha ndipo Akaanzisha gazeti la Habari Leo.
" Nirudie Tu Sisi habari Leo nikiwa Mhariri ilikuwa baada ya Shule moja kukamilika tulitoka na kichwa cha habari mara kadhaa kisemacho Shule nyingine ya Lowasa yakamilika", anasema Mluma
(Kushoto) Betty Mkwasa akiwa kwenye Mkutano Mkuu wa Vyombo vya Utangazaji Nchini Uliofanyika Jijini Dodoma.
Kwa Upande wake aliyewahi Kuwa Mkuu wa Wilaya wakati Lowasa akiwa Waziri Mkuu, Betty Mkwasa ambaye pia NI Mjumbe wa Kamati hiyo Inayosimamia Maudhui TCRA Kwa Sasa, anasema mara ya Kwanza alimfahamu Hayati Edward Lowasa wakati yeye akiwa mwandishi na Mtangazaji wa RTD, Itv na Radio one
"Hayati Lowasa aliwapenda na kuwathamini waandishi wa habari, ilikuwa kwenye ziara zake anahakikisha wanakuwa salama, wanakula na kulala vizuri,
alipenda pia habari zake ziandikwe na kuripotiwa vizuri, alikuwa anapiga simu kuulizia na kumsema mwandishi aliyekosea kuandika habari za Lowasa", amesama Mkwasa
Aidha Mkwasa anasema Wakati yeye akiwa mkuu wa Wilaya Waziri Mkuu Lowasa aliwasimamia kwa Karibu mno, na kusema kweli walimuogopa kwani hakuwa anataka mchezo kazini.
"Katika Kipindi hicho Sisi tukiwa Wakuu wa Wilaya ndipo hizi shule za Sekondari za kata zilianzishwa, tulifanya Kazi kubwa mno katika ujenzi huo ambapo Lowasa alitaka kila Mkuu wa wilaya aripoti kwake moja kwa moja kuhusu maendeleo ya ujenzi huo,
Ili kuwa ikitokea Kusuasua kwa ujenzi wakuu wa mikoa bila kujali ni mkoa gani alipo, aliitwa kujieleza Ofisini kwa waziri Mkuu Dar es lama", amesema
Kuhusu Siasa Betty anamzungumza Hayati Lowasa Kuwa alikuwa mpenda haki
"Unajua kwenye Siasa Kuna Majungu, Fitna, Uonezi na kuzushiana Sana, lakini Lowasa alikuwa mkweli na alitoa haki kwa kila aliyestahili kuipata bila kusikiliza majungu", amesema
Leo Februari 16,2024 heshima za Mwisho zimetolewa jijini Arusha, wakati wa kuuaga mwili wa hayati Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowasa ambao Utazikwa Kesho nyumbani kweke Monduri..!!!