BANDA MEDIA BLOG

MAAJABU YA MWANAMKE KUIBADILISHA JAMII KWENYE MATUMIZI YA NISHATI SAFI NA SALAMA YA KUPIKIA - DKT. BITEKO

 





JUMAMOSI Machi 9, Makamu wa Rais Dkt. Phillip Isidori Mpango ameshiriki Kongamano la wanawake kuhusu nishati safi ya kupikia Kongamano lililoandaliwa na wizara ya Nishati likifanyika jijini Dodoma na kuhudhuriwa pia na naibu waziri mkuu na waziri wa Nishati Dkt. Doto Biteko katika ukumbi wa mikutano wa JAKAYA KIKWETE

Naibu waziri Mkuu na waziri wa Nishati,  Mhe. Biteko amesema katika kuleta mabadiliko ya Matumizi ya Nishati Safi na Salama mwanamke mwenyewe anatakiwa kuwa mstari wa mbele

" kwenye ajenda hii batani ya kuleta mabadiliko ya nishati safi ya kupikia hapa Nchini ni mwanamke mwenyewe wa Tanzania",

 "Huyu akiweza kuibeba ajenda akaichukua kama ajenda yake watu wengine watafuata",

"Mungu amempa uwezo wa pekee, uwezo wa kibaiolojia lakini na upana wa ubongo wao,  amemuumba kwa namna ya ajabu sana ,tena ya kupendeza",

"Amempa tumbo si tu linatumika kwenye mmeng'enyo wa chakula bali limebeba uhai wa binadamu ndani yake,  Mungu amempa uwezo mwanamke wakufanya Jambo zaidi ya moja 

kwa wakati mmoja tofauti sana na mwanaume "

"Mungu amempa uwezo mwanamke wa kusema kidogo na kutenda zaidi ,Mungu amempa uwezo mwanamke wakuwa sababu ya furaha kwa viumbe wengine Duniani

"Kwakweli kama unamwanamke aliyewezeshwa anayejali nishati safi ya kupikia 

hutatumia muda mwingi kuzungumzia nishati safi ya kupikia the bali mwanamke ataisukuma ajenda hii" amesema Dkt. Dotto Biteko

Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG