BANDA MEDIA BLOG

MISIKITI ITUMIKE KUTATUA CHANGAMOTO ZA JAMII- RAIS MWINYI


RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Alhaj Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema Misikiti itumike kutatua changamoto zilizopo katika jamii.

Rais Dk.Mwinyi amesema hayo alipojumuika na Waumini wa Dini ya Kiislamu katika ibada ya Sala ya Ijumaa na kufungua Msikiti wa Masjid Itiswaam Kizimkazi Mkunguni, Mkoa wa Kusini Unguja tarehe: 8 Machi 2024.

Aidha Rais Dk.Mwinyi amewahimiza Waumini wa Dini ya Kiislamu kuitumia Misikiti kufanya ibada kwa wingi hususani kuelekea kipindi cha Mwezi Mtukufu wa Ramadhan. 

Kwa upande mwingine Rais Dk.Mwinyi amesema kuna wajibu wa kuwafundisha watoto elimu ya Dini mapema.

Halikadhalika Rais Dk.Mwinyi amewataka waumini kuendelea kumuomba Mwenyezi Mungu kudumisha amani, upendo, umoja na mshikamano.

Rais Dk.Mwinyi ametoa shukrani kwa wafadhili waliofanikisha ujenzi wa Msikiti huo.


Masjid Itiswaam, Kizimkazi Mkunguni Mkoa wa Kusini Unguja.







Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG