BANDA MEDIA BLOG

RAIS DKT. MWINYI AENDELEA KUPOKEA SALAMU ZA POLE

 


Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amepokea salamu za pole nyumbani kwake Ikulu Migombani kutoka kwa Naibu Waziri Mkuu Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dotto Mashaka Biteko, Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe. Hemed Suleiman Abdullah ambaye ameongozana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Katiba Sheria Utumishi na Utawala Bora Mhe. Haroun Ali Suleiman, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Mohamed Mussa, Katibu wa Baraza la Mapinduzi na Katibu Mkuu Kiongozi Mhe. Zena Ahmed Said. Baadae alifika Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Mhe. Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Pili Mstaafu Mhe. Balozi. Seif Ali Iddi kufuatia kifo cha Aliyekuwa Rais wa Zanzibar na Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu Marehemu Mzee Ali Hassan Mwinyi ambaye amefariki dunia tarehe: 29 Februari 2024 katika hospital ya Mzena, Dar es Salaam na kuzikwa Mangapwani tarehe: 02 Machi 2024.




Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG