BANDA MEDIA BLOG

RC. SENYAMULE AFUNGUA WIKI YA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI

 

Rc. Senyamule akipokea zawadi ya Vitabu toka kwa mtendaji mkuu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Ester Masego

NA JOHN BANDA, DODOMA

MKUU wa Mkoa wa Dodoma  Rosemary Senyamule Amewataka Watumishi wa Taasisi za Serikali  Kubandika matangazo yasemayo Kero yako Wajibu Wangu na kuyabandika kwenye mbao zilizopo kwenye mbao za matangazo ili kuwapa Uhuru wananchi wa kujua wanahudumiwa na ofisi yoyote ya serikali

 Senyamule Ametoa Agizo Hilo Leo Machi 07, 2024 wakati akifungua maonesho ya maadhimisho ya siku ya wanawake Duniani katika Uwanja wa Mashujaa Jijini Dodoma.

Amesema kila afisa ahakikishe anatoa huduma Kwa wananchi katika ofisi yake, ili pia kutowafanya Wananchi kukosa Imani na ofisi zenu kisha kuamua kukimbilia Ofisini ya Mkuu wa Mkoa kuja kuleta kero zao

"Inasikitisha Sana kuona ofisi za serikali zipo kila mahali lakini mwananchi anaamua kufunga safari kutoka Kilometa Nyingi Kwenda kutafuta Msaada katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa", Amesema

Akiongelea Kuhusu Maonyesho hayo ameshauri wananchi kuchangamkia Fursa  ya kwenda katika viwanja vya  Mashujaa ili kupata elimu mbalimbali ikiwemo kutatuliwa Kero zao na wataalamu mbalimbali waserikali waliopo kwenye mabanda hayo.

" Kama tulivyoambiwa hapa katika uwanja wa Mashujaa kuna Mabanda ya Maonyesho 53, ya Wataalamu kutoka katika Wizara tofauti za serikali, Mkoa na wilaya pamoja na wanawake wajasiriamali ambao wanaonyesha na kuuza bidhaa Zao", amesema

Ameongeza kuwa Maonyesho hayo yatakuwa ya siku 5 kuanzia Leo na kwamba yatahimishwa Machi 11.

Awali Mkuu huyo wa mkoa aliyatembelea Mabanda hayo ili kujionea Kazi mbalimbali zinazofanywa na Taasisi hizo. ambapo Afisa Mtendaji Mkuu wa  Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Africa Mashariki, Ester Masego amesema pamoja na mambo mengine Wana Taasisi ya EPRM ambayo inakusanya na kutoa Taarifa zinazosaidia wanawake.







Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG