BANDA MEDIA BLOG

VYAMA VYA USHIRIKA VINALIPA WANAWAKE WAITWA KUJIUNGA

 

Mkurugenzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tahini wa TCDC Flora Bilauri akizungimza Jambo na waandishi wa habari.

RC. Dodoma alipotembelea Banda Tume ya Ushirika wakati wa ufunguzi wa maonyesho hayo

NA JOHN BANDA, DODOMA

WANAWAKE Nchini wametakiwa kujiunga na vyama vya Ushirika ili kurahisisha shughuli zao za Maendeleo Kwani kujitenga na kufanya  kwa Mtu mmoja mmoja Ni Sawa na kujitengenezea Udhaifu

Wito Huo Umetolewa na Mkurunzi wa Mipango, Ufuatiliaji na Tathimini wa Tume ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania (TCDC), Flora Bilauri wakati akiongea na waandishi wa habari kwenye Banda la Tume hiyo lilipo katika Uwanja wa Mashujaa jijini Dodoma.

Bi. Flara amesema wanawake watakapokuwa pamoja na Kufanya Shughuli zao katika Ushirika, Matokeo ya Kiuchumi na Kimaendeleo yatakuwa ni Makubwa.

"Nawahakikishia wanawake kuwa chochote ambacho watakifanya wakiwa ndani yaushirika kitakuwa na matokeo makubwa na ya uhakika", amesema

Aidha amesema kitendo cha TCDC kushiriki Maonyesho hayo ni kuitika wito wa serikali ulizitaka taasisi za serikali kushiriki, lakini pia kuutangaza ushirika na faida zake kwa wanawake

Ameongeza kuwa wameamua kuutangaza ushirika ili kuwaunganisha wanawake na fursa mbalimbali pamoja na kuwakutanisha na wawezeshaji wengine 

Mabanda 53 ya maonyesho ya shughuli mbalimbali yapo katika uwanja huo wa mashujaa jijini Dodoma yakijumuisha wizara, taasisi za serikali na wajasiriali ambapo maonyesho haya yatafungwa Machi 11 Mwaka huu.



Post a Comment

Previous Post Next Post
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG
BANDA MEDIA BLOG