NA JOHN BANDA, DODOMA
NAIBU Waziri Mkuu Dtk. Dotto Biteko Usiku wa Jumamosi Machi 9,2024 Amezindua Hotel ya Rafiki iliyopo Jijini Dodoma Huku akiwataka watendaji wa Serikali Kuondoa Urasimu katika kuwahudumia Wananchi.
"Nitoe wito Kwa watendaji wa Serikali nikiwemo Mimi Mwenyewe kuwa tuhakikishe tunawahudumia wananchi kwa wakati wanapohitaji huduma
Ifike Mahali tuone aibu, tuna wajibu wa kulea Sekta Binafsi, mfano Maji, Umeme ,vibari vya ujenzi na idara nyingine Kazi tunayoweza Kuifanya Leo kwanini umwambie mtu aje kesho?? tuache urasimu usio na sababu, yeye ajuaye kutenda mema asiyatende kwake Mtu huyo itakuwa ni dhambi", amesema na kusisitizi
Aidha amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan amefurahishwa na uwekezaji unaofanywa jijini Dodoma ambapo ni Makao makuu ya Nchi, na kwamba amejipambanua kwa kuwa mlezi wa sekata binafsi hivyo asingependa kuona wafanyabiashara na wananchi wananyanyasika Kwa namna yoyote.
Kwa Upande wake Mtendaji Mkuu wa Rafiki Hoteli Fladmiry Mallya ameishukuru Serikali kwa Kuweka Mazingira Mazuri ya Uwekezaji yanayomsaidia kila Mtanzania Kuwekeza kwenye Nchi yake.
naye Meneja Usambazaji wa Hotel hiyo Fred Zayumba, amesema Hotel hiyo ina Jumla ya vyumba 80 vyenye ubora Tofauti, kumbi 4 za mikutano, Bwawa la kuogelea, Usafiri kwa wageni, baa na sehemu kubwa ya maegesho ya magari , ambapo Watanzania 60 wamepata ajira rasmi na 50 zisizo Rasmi, Hotelini hapo.
Zayumba ameongeza Kuwa ni pamoja na malazi, Chakula na vinywaji vinavyopatika katika hotel hiyo pia kuna Bwawa la kuogelea, Internet na Chumba cha Mazoezi.
pia ameishujuru serikali kwa kushirikiana Bega kwa Bega kwa ukaguzi wa mradi huo wakati wa ujenzi pamoja na kutoa ajira kwa hizo kea watanzania ambapo wao watahakikisha wanatoa huduma Bora kwa wateja wa ndani na nje ya Nchi.



