Katika taarifa, msemaji wa Jeshi la
Polisi la nchi hiyo Paul Nyathi anasema Ishmael Chokurongerwa, mwenye miaka 56,
anaongoza kikundi cha wafuasi zaidi ya 1,000 wanaokutana katika shamba maalumu,
lililoko takribani kilomita 34, kaskazini magharibi mwa mji mkuu wa nchi hiyo,
Harare.
Kulingana na Nyathi, watoto hao walikuwa
wanatumikishwa katika shughuli ngumu kwa manufaa yake mwenyewe. Kati ya watoto
251, 246 hawakuwa na vyeti vya kuzaliwa.
“Polisi wamegundua kuwa watoto hao wenye
umri wa kwenda shule, hawakupata elimu rasmi na walitumikishwa kwenye kazi
ngumu,” anasema Nyathi.
'Vitendo vya kihalifu'
Kati ya makaburi hayo, saba yalikuwa ni
ya watoto wachanga ambao vizazi vyao havikuwa vimesajiliwa.
Kulingana na Nyathi, maofisa polisi
walivamia eneo hilo siku ya Jumanne. Chokurongerwa, anayejiita Nabii Ishmael
alikamatwa akiwa na wasaidizi wake kwa kuendesha matukio ya uhalifu dhidi ya
watoto.”
Nyathi amesema taarifa zaidi juu ya
uchunguzi wa tukio hilo unaendelea na utatolewa ndani ya siku chache.
Gazeti la H-Metro, ambalo lilikuwa sehemu
ya operesheni hiyo, walionesha picha za polisi waliovalia mavazi maalumu,
wakibishana na waumini wanawake waliokuwa wakishinikiza kuchukua watoto wao
waliokuwa wamewekwa kwenye basi la polisi. Haikufahamika mapema sababu ya polisi
kuwazuia watoto hao.
'Hakuna elimu'
“Kwanini wanawachukua watoto wetu?
Tumeridhika kuwepo hapa. Hatuna tatizo lolote,” alilalamika mwanamke mmoja
kupitia video mjongeo iliyowekwa kwenye mtandao wa X.
Kulingana na gazeti hilo, polisi walikuwa
na silaha, mabomu ya machozi na mbwa walivamia eneo hilo la makaburi ambalo
wanaliita kama "nchi yao ya ahadi."
Mmoja wa wasaidizi wa Chokurongerwa
alifanyiwa mahojiano na gazeti hilo.
“Imani yetu haitoki kwenye maandiko,
tumeipata moja kwa moja kutoka kwa Mungu aliyetupa sheria za kuingia mbinguni.
Mungu anakataza elimu kwani yanayofundishwa yanakwenda kinyume na maagizo
yake,” alisema, na kuongeza “Mungu alituambia mvua haitonyesha kama
tutawapeleka watoto wetu shule. Ona hali ya ukame ilivyo, na sisi tunapata mvua
hapa. Tumepata zawadi ya sikio la kiroho ya kusikiliza sauti ya Mungu,”
alisema.
'Kushinda njaa mpaka kifo'
Makundi ya kitume ambayo yanaingiza imani
za kimapokeo katika fundisho la Kipentekoste ni maarufu katika nchi hiyo ya
kusini mwa Afrika yenye kidini.
Kumekuwa na utafiti mdogo wa kina kuhusu
makanisa ya Kitume nchini Zimbabwe, lakini tafiti za UNICEF zinakadiria kuwa
ndilo dhehebu kubwa zaidi la kidini lenye wafuasi karibu milioni 2.5 katika
nchi yenye watu milioni 15. Baadhi ya vikundi hivyo vinazingatia mafundisho
yanayowataka wafuasi kuepuka elimu kwa watoto wao pamoja na dawa na huduma za
matibabu kwa wanachama ambao wanapaswa kutafuta uponyaji kupitia imani yao
katika sala, maji matakatifu na wapakwa mafuta.
Katika miaka ya hivi karibuni, baadhi yao
wamewaruhusu wafuasi wao kutembelea hospitali na kuwaanzisha watoto wao shule,
kufuatia kampeni mfululizo kutoka serikalini na taasisi zisizo za kiserikali.
Aprili mwaka jana, Kenya ilimkamata
mchungaji aliyesemekana kuwalazimisha wafuasi wake washinde njaa ili waweze
kumuona Yesu.
Mwendesha mkuu wa Mashitaka wa nchi hiyo
aliagiza mchungaji Paul Mackenzie na wenzake 90 washitakiwe kwa mauaji ya
wafuasi wao 429, ukatili na utesaji.
