...............................................................................................
NA JOHN BANDA, DODOMA
Viongozi wa Taasisi ya Kumuombea Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania na wasaidizi wake Aprili 5,2024 wamekutana na kufanya Maombi ya
Kuliombea Taifa Bungeni jijini Dodoma.
Akiongea na Waandishi wa Habari mara baada ya Maombi
hayo Katibu mkuu wa Taasisi hiyo Dkt. James Lukuba amesema lengo kubwa ni kumuombea
Rais na wasaidizi wake ili waweze kutenda haki wanapowatumikia wananchi
wanaowaongoza.
“tunalenga taifa letu la Tanzania liwe na amani, liwe
na viongozi bora wanaojali maslahi ya wananchi wao wanaowaongoza kwa kuwatendea
haki”, amesema
Aidha amesema kongamano hilo ni la pili kuwakutanisha
waombaji kupitia jukwaa hilo, ambalo ni mwanzo tu wa kutengeneza njia ya amani
kwa watanzania na viongozi wao, amani ni pale wananchi watakapojua thamani ya
Nchi yao, amani ni pale watanzania watakapojua thamani ya Viongozi wao na kujua
chakufanya ili waweze kuitunza amani iliyopo Tanzania ambayo chanzo chake ni
Mungu mwenyewe.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Taasisi hiyo ambaye Pia
ndiyo Mmbeba maono Peter Shariff Abubakary amesema kazi kubwa ya wajumbe wa taasisi hiyo ambayo
inajumuisha viongozi na waumini wa Dini mbalimbali hapa nchi nikuomba tu.
“Jumla ya wanamaombi hawa wapo 5,752 wakipatikana zaidi
ya mikoa 22 ya Tanzania huku waliokutana Bungeni Dodoma ni zadi ya 200, kutoka
ngazi ya wilaya, mikoa na taifa.”, amesema
Naye katibu Mkuu wa taasisi hiyo Zanzibar Angelina Adam Malembeka amesema
wao ni wanajeshi wa Kiroho kwa ajili ya Kuwalinda viongozi Pamoja na wananchi.
“sisi
ni wanajeshi wa kiroho, wakati wanajeshi na askari wengine wanalinda viongozi Pamoja
na wananchi kupitia sira za moto, sisi ulinzi wetu tnaufanya kiroho kwa njia ya
maombi”, amesema
Viongozi
wanaenda vizuri, wanafanya vizuri miradi ipo tunaona inatekelezeka, lakini sisi
tunawaombea ili kuwatia nguvu, tunahitaji upendo katika jamii na viongozi”,
amesema